Jumanne, 5 Mei 2015
barbra william
Hatari sana! Mkali wa Ngoma ya Chekecha Cheketua, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ amenusurika kifo baada ya kuvamiwa nyumbani kwake na majambazi ambao walimteka mlinzi na ndugu yake mmoja kisha kuwashushia kibano kikali huku wakiwaamuru wawapeleke kwenye chumba anacholala msanii huyo,Akizungumza kwa masikitiko makubwa na mwandishi wetu Mei 2, mwaka huu, Abdul Kiba ambaye ni mdogo wa Ali Kiba, alisema usiku wa siku ya tukio alipewa taarifa na Ali Kiba kuwa amevamiwa na majambazi wenye silaha za moto hivyo alikurupuka moja kwa moja hadi Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar ambapo waliripoti na baadaye kupata msaada wa polisi hadi eneo la tukio nyumbani kwa jamaa huyo Kunduchi Beach.
“Wakati linatokea tukio hilo nilikuwa Masaki (Dar) na jamaa yangu mmoja anaitwa Bude, kaka (Ali) alinipigia simu na kuniambia kilichotokea nasi hatukuchelewa tukaenda polisi na kuwaeleza hivyo tukaambatana nao hadi nyumbani.
“Tulikuta wamevunja mlango na kuzama ndani ambapo chumbani kwangu walichukua tivii flat screen, viatu na nguo zangu, maana kumbe wakati wanaenda chumbani kwangu walijua ni chumba cha Ali.
“Bahati nzuri majambazi walipofika walimwambia yule ndugu yetu aliyekuwa pamoja na mlinzi awaelekeze chumba cha Ali ambapo aliwapotosha kwa kuwaelekeza kwangu.
“Baada ya kuvunja mlango hawakumuona hivyo wakamuuliza akawaambia hajui labda katoka yeye akiwa amelala ndiyo wakaishia kuchukua vitu hivyo vya ndani.
“Wakati wanafanya hayo yote yeye (Ali Kiba) alikuwa akiwasikia tu chumbani kwake maana hadi wanatoka alikuwa akiwafuatilia kwa makini na hata maneno waliyokuwa wakizungumza yalikuwa yakutishia sana amani yake.
“Nashukuru kaka yangu hajaguswa, ila wameiba vitu kibao maana ukiachilia mbali tivii yangu na nguo wamechukua tivii ya sebuleni na kila kitu kilichobebeka,” alisema Abdul Kiba.
Hadi storyi hili inakwenda mitamboni, jeshi la polisi lilikuwa likiendelea na uchunguzi wa kuwasaka watuhumiwa.
Ni vyema mastaa mbalimbali ambao wanaonesha mali zao kama Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wakaimairisha ulinzi nyumbani kwao ili kujilinda zaidi. -Mhariri
photo by:global publishers
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Search
Popular Posts
-
Msanii wa filamu nchini ambaye pia ni Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu, kufungua duka kubwa la urembo nchini Afrika Kusini. Kwa mujibu wa c...
-
WENGI ukiwauliza kuwa wanamfahamu vipi Kojate Mwegelo, jibu lao litakuwa ni Mshindi wa pili wa Miss Tanzania mwaka 2006. Wengine ...
-
Hii ni baada ya taarifa siku ta jana kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na watu wengi kushangaa kwanini Miss Tanzania 2020-2021 Rose...
-
ALLY REHMTULAH KUJA NA UFAHARI WETU FESTIVAL Mbunifu wa mavazi nchini Tanzania Allyrehmtullah ameandaa tamasha linalokwenda kwa jina ...
-
KAA UKITAMBUA KUWA MKE NI MATUNZO, YAANI SAWA NA MGOMBA KUPALILIWA KILA WAKATI!!! Assalaam alaikum/Bwana Yesu asifiwe! Bila shaka mna afya ...
-
Msanii wa Movie hapa nchini Elizabeth Michel a.k.a Lulu amefunguka haya mambo matano kuhusu chama anachokipenda na ni nani atampigia kura...
-
Akiwa na umri wa miaka 89 aliishi katika kipindi kigumu katika miaka ya 1990 kutokana na talaka za watoto wake 3 na ukimya usiokifani...
-
MISS KINONDONI 2019 PRESS BONANZA Leo miss kinondoni wamefanya special bonanza kwa lengo la kuchangia kituo ch...
-
Tarehe kama ya leo julai 18 mwaka 1918 alizaliwa,Mzee Nelson Mandela Raisi wa kwanza wa Africa kusini alichaguliwa kidemokrasia na ni mshind...
-
JINSI YA KUMTAMBUA MWANAMKE ANAYEKARIBIA KUKUACHA! Kuna tofauti kubwa ya kimaamuzi kati ya mwanaume na mwanamke kwenye suala la k...
Recent Posts
Categories
Sample Text
Blog Archive
-
▼
2015
(56)
-
▼
Mei
(12)
- Kwa nini wanaume hutoa mamilioni ya manii katika k...
- Hisia nane hatari katika mapenzi
- Aina 10 ya Wanawake Wanaopendwa na Wanaume
- Hatua 5 za kuzungumza na mpenzi wako aliyekasirik...
- JINSI YA KUMTAMBUA MWANAMKE ANAYEKARIBIA KUKUACHA...
- MESEJI NZURI ZA MAPENZI KWA UMPENDAYE KWA DHATI ...
- Updated Eyebrow Tutorial
- DIY Turn Your Old Pants Into Cool Bleached, Distre...
- BEYONCE has outdone Kim Kardashian’s and Jennifer ...
- A-Z ALI KIBA ALIVYONUSURIKA KUUAWA!
- Mashabiki wa Wema Sepetu na Diamond Platnumz..Matu...
- SHETTA “NAMUOMBA MUNGU ANGEMLETA ROSE NDAUKA MAPEM...
-
▼
Mei
(12)
0 maoni:
Chapisha Maoni