Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Afya. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Afya. Onyesha machapisho yote
Alhamisi, 20 Agosti 2015
Kufanya Ngono ama mapenzi si tu kujihisi au kujisikia vizuri. Pia inaweza kuwa nzuri kwa ajili yenu. Hapa ni kile ambacho maisha ya kimapenzi kiafya yanaweza kufanya kwa ajili yenu au yako. Soma zaidi ufahamu faida hizi za kushangaza.
1. Husaidia kuweka mfumo wa kinga yako vizuri
"Watu walio imara katika ngono kuchukua siku chache kuwa wagonjwa," anasema Yvonne K. Fulbright, PhD mtaalam wa afya ya ngono.
Watu wanaofanya mapenzi huwa na kiwango cha juu cha kinga ya mwili wao dhidi ya wadudu, virusi, na wavamizi wengine katika mwili.
Watafiti katika Chuo Kikuu cha Wilkes huko Pennsylvania iligundua kuwa wanafunzi wa chuo ambao walikuwa wakijihusisha na ngono mara moja au mbili kwa wiki walikuwa na kiwango cha juu cha kinga ya mwili ukilinganisha na baadhi ya wanafunzi waliokuwa wamefanya ngono chini ya mara kwa mara.
Kumbuka
Unapaswa bado kufanya mambo mengine ili kwamba kufanya mfumo wako wa kinga na uwe imara, kama vile:
- Kula vizuri.
- kuwa imara / kufanya mazoezii.
- Kupata usingizi wa kutosha.
- Kuweka au kufanya chanjo kadiri inavyotakiwa.
Pia katika mapenzi
Matumizi ya kondomu kama hamjuani wote kuhusu hali magonjwa ya zinaa yako baina yenu. Ili kujikinga na afya zenu kwa kujiepusha na hayo magonjwa yanayoweza kushusha kiwango cha kinga ya mwili wako.
2. Inaongeza hamu ya kufanya mapenzi zaidi/ boosts libido
"Kwa kufanya ngono, hufanya ngono kuwa bora na kuboresha hamu yako ya kufanya mapenzi tena na tena ," anasema Lauren Streicher, MD. Yeye ni msaidizi kliniki profesa wa masuala ya uzazi na magonjwa ya wanawake katika Chuo Kikuu cha Northwestern Feinberg katika Shule ya Tiba huko Chicago.
Kwa wanawake, baada ya ngono hufanya uke kupata vilainishi /lubrication, mzunguko wa damu yake katika mwili, na utanukaji wake, anasema, hivi vyote ni baada ya kufanya ngono humfanya mtu kujisikia vizuri na kusaidia kutamani zaidi na hivyo kumwongezea hamu zaidi ya kusisimua katika suala zima la mapenzi!!
3. huimarisha cha kibofu cha mkojo kwa Wanawake.
Uimara wa nyonga/pelvic ni muhimu kwa ajili ya kuzuia madhaifu hayo, Kitu ambacho huathiri karibu ya wanawake 30% wakati fulani katika maisha yao. Ngono nzuri ni kama kazi ya kuimarisha misuli ya kiuno au nyonga. Wakati una upofika kileleni/mshindo, kwa sababu ukazaji wa misuli yake, hufanya kuimarisha kwa kibofu.
4. Hupunguza shinikizo la damu.
Utafiti unaonyesha uhusiano kati ya ngono na kupunguza shinikizo la damu, anasema Joseph J. Pinzone, MD. Yeye ni Mkurugenzi Mtendaji na mkurugenzi wa tiba katika chuo cha Amai.
"Kumekuwa na tafiti nyingi," anasema. "Moja ya utafiti wa kihistoria ulibaini kuwa kujamiiana hasa (si Punyeto) hupunguza sytolic shinikizo la damu." na hiyo ndio kipimo cha ya kwanza cha shinikizo la damu.
5. Huhesabika kama moja ya Zoezi
"Ngono ni aina moja kubwa sana ya zoezi," Pinzone anasema. Japokuwa haiwezi kuchukua nafasi kama ya mashine ya kufanyia mazoezi yale ya kukimbia au kutembea huku upo pale pale (treadmill), lakini huwa inakuwa umefanya kitu fulani.
Ngono hutumia kalori zipatazo tano kwa dakika, ili hali kalori nne zaidi kuliko kuangalia TV. Inakupa nguvu ya ngumi 1-2: Pia huupa moyo kasi yake kwenda vizuri na pia kutumia misuli mingine mbalimbali kufanya kazi.
Hivyo kuwa busy! Unaweza kuwa na muda wako na ratiba ya kufanya mazoezi mengine mara kwa mara. "fanya mazoezi, kwa uthabiti husaidia kukuuongeza faida," Pinzone anasema.
6. hupunguza hatari ya kupata shambulio la moyo.
Maisha mazuri ya ngono ni mazuri pia kwa moyo wako. Licha ya kuwa njia nzuri ya kuongeza kiwango cha ufanisi wa moyo wako, ngono husaidia kuweka estrogen yako na kiwango cha Testosterone katika uwiano sahihi.
"Wakati mmoja au miongoni mwa hizo homoni unapokuwa chini hupelekea kusababisha kwa kupata kwa matatizo mengine kujitokeza, kama osteoporosis na hata ugonjwa wa moyo," Pinzone anasema.
Kufanya ngono mara nyingi zaidi inaweza kukusaidia. Wakati wa utafiti mmoja hivi, watu waliokuwa wamefanya ngono angalau mara mbili kwa wiki wako vizuri, ingawa kuna uwezekano wa kufa na ugonjwa wa moyo kwa watu ambao hufanya ngono mara chache zaidi.
7. Hupunguza maumivu ya mwili
Kabla ya kufikiria panadol au aspirin, jaribu kufika kileleni au mshindo katika mapenzi.
"kilele au mshindo unaweza kuzuia maumivu," anasema Barry R. Komisaruk, PhD, Profesa, Chuo Kikuu cha New Jersey State.
Inazitoa homoni ambayo husaidia kuongeza maumivu yako kupindukia.
"Imegundulika kuwa kusisimua uke kunaweza kuzuia usugu na maumivu ya mguu, na wanawake wengi wametuambia kuwa sehemu za siri binafsi kusisimua kunaweza kupunguza maumivu ya tumbo la hedhi, na katika baadhi ya kesi hata maumivu kuumwa na kichwa hupungua," Komisaruk anasema.
8. Inaweza kupunguza uwezekano wa kupata kansa ya tezi dume / Prostate Cancer
Ngono inaweza kusaidia kuizuia saratani ya kibofu.
Watu ambao hukojoa mara kwa mara (angalau mara 21 kwa mwezi) huwa wako katika kiwango cha chini cha uwezekano wa kupata kansa ya kibofu wakati wa utafiti moja ulisema, ambayo ulikuwa ukichapishwa katika jarida la American Medical Association.
Haieleweki wazi kuwa ngono ndiyo sababu tu ambayo linaogopwa katika utafiti. Pia kuna mambo Mengi ambayo huathiri zaidi na kuchochea hatari ya kansa. Lakini si ngono tu.
9. Inaboresha hali ya usingizi
Unaweza kukubali kwa haraka zaidi baada ya ngono, na kwa sababu nzuri. "Baada ya kufika kileleni au mshindo, homoni ya prolactin hutolewa, ambayo hujihusisha na hisia ya utulivu na usingizi" baada ya ngono, anasema Sheenie Ambardar, MD Mtaalamu wa magonjwa ya akili huko West Hollywood, Califonia.
10. HUPUNGUZA MSONGO WA MAWAZO
Kuwa karibu na mpenzi wako kunaweza kupunguza mawazo na wasiwasi.
Ambardar anasema kugusana na kukumbatiana inaweza kusababisha kutolewa kwa vitu asilia vya mwili "homoni za kujisikia-vyema."
Vile vile hisia za kimapenzi husababisha kutolewa kwa kemikali katika ubongo ambayo huunufaisha ubongo katika mfumo wake mzima. Mapenzi na urafiki wa ndani unaweza kuongeza kujithamini kwako na kuwa na furaha pia, Ambardar anasema. Si tu inaelezewa katika masuala ya kiafya, lakini ni moja ya furaha.
Ijumaa, 17 Julai 2015
Miti shamba inayofanya matiti kuwa makubwa na yaliyosimama


MATITI ya mwanamke kuwa katika shepu bomba ni shauri la wanawake wengi na si shauri la mtu mmoja tu. Aidha ni sehemu ya mwili wa mwanamke inayotoa msisimko mkubwa.
Wapo wanawake ambao wana musuli nyingi za matiti na hivyo wanakuwa na matiti makubwa na wengine wana kiasi kidogo na hivyo kuwa na matiti madogo.
Hali hiyo ina sababu zake ingawa wataalamu wanasema kwamba ukubwa wa maziwa huambatana na historia ya familia, umri,kupungua kwa uzito, ujauzito unene na kunyumbuka kwa ngozi ya kwenye matiti, kiwango cha homoni hasa estrogen na progesterone.
kwa kuwa matiti ya mwanamke ni sehemu ya utambuzi wake wa ukike na mwenyewe alivyo na pia ni alama ya uzazi na salama kwa mtoto wake.
Uzuri wa matiti ni kuwa mazima na kama kukitokea kasoro kidogo tu huwa ni kasheshe kubwa kwa upande wa mwanamke. Kutokana na hili nashauri wanawake kuwa na tabia ya kutunza matiti yao ikiwa ni pamoja na kuyakagua na kama kuna kasoro kuyafikisha kwa wahusika kuangalia tatizo.
Usafi wa mwili huambatana na kuyatunza vyema matiti yako.
Lakini wengi wanaotaka matiti makubwa ndio ho wanaopata adhabu ya kusaka matiti hayo kwa udi na uvumba.
Uzuri wa matiti
zipo njia nyingi za kuwa na matiti bomba na kwa sasa duniani matiti bomba ni yale makubwa( nadhani hii ni fasheni).Unaweza kupata matiti hayo kwa upasuaji au na kwa kupachika kitu ndani hasa silikoni na nyingine ni kutumia dawa ambapo misuli hujazia na kuyafanya matiti kuwa makubwa.
Njia ya kukuza matiti kwa salama ni kutumia dawa ambazo zimetolewa katika miti shamba, mitishamba ambayo ikichanganywa pamoja inafanyakazi mbalimbali ya kuboresha ukubwa na uimara wa matiti.
Mitishamba hii inatoka sehemu mbalimbali na Afrika Kusini wamefanikiwa kutengeneza dawa kutokana na miti hii na wanaotaka urembo wa matiti makubwa na yenye kuonekana wanapata nafasi kubwa ya kununua dawa hiyo.
Aidha baada ya kujazia matiti yako na kuwa makubwa kitu kinachofuata ni kuhakikisha kwamba matiti yako hayalegei na kuwa katika ukubwa wake bado yanasimama katika saa inayotakiwa na yenye raha yake si kutazama bali pia kuyatomasa.
Matiti hupendeza zaidi baada ya kuonekana yakiwa yametulia na yanayokubali brasia zenye maana duniani.
Aidha uzuri mwingine utatokana na kuwezesha matiti yako imara kwa kufanyia hali ya kuwezesha musuli za maziwa kufanyakazi yake.
Pamoja na kuongeza ukubwa wa matiti ni vyema kama ngozi yako inakuwa na rangi ile inayofaa huku ukihakikisha kwamba chini ya maziwa jacho halikai na wala brasia haisababishi wewe kuwa na kazi ya ziada katika usafi wa eneo hilo.
Ipo haja ya kutumia mafuta yanayostahili kukata mnururisho mkali wa mwanga unaoweza kusababisha kansa ya ngozi.
Kliniki moja ya Afrika Kusini St Herb Beauty Breast Care imetengeneza aina fulani ya mitishamba yenye mchanganyiko maridhawa kwa ajili ya matumizi ya wanawake wanaotaka urembo wa matiti makubwa na yaliyosimama bila upasuaji wala kutumbukiza kitu katika matiti hayo.
Ni lazima kuwe na mizania ya mitishamba kupata kile kitu unachotaka. Kliniki hiyo imekuja na fomula yake inayoitwa Beauty Bust Herbal Breast Enlargement Formula ambayo hushawishi kukua kwa misuli za matiti bila kushawishi uzalishaji wa maziwa na kuyaongezea uzuri matiti yako.
Pamoja na matiti hayo kuwa bora kwa matumizi hayo, matiti makubwa hulainika sana unapokuwa mzee na hili ndilo hasa nililotaka kusema, mazoezi ya mwili husaidia sana bado kuweka matiti katika shepu yake.
Kama u kijana na matiti yako yanakuwa malapa basi huenda tatizo si tu musuli zimelegea bali pia huvai brasia kukusaidia. maziwa yanaweza kuwa malapa kwa kutokuwa na kitu cha kusaidia kusimama.Hili ni wazi zaidi kwa wanawake wenye matiti makubwa au watu ambao wanafanya mazoezi bila kuwa na sapoti ya brasia.Pia matiti yanaweza kuwa malapa kutokana na kujifungua
Lakini ukitaka uhakika wa uzuri wako kwa namna ya kuwa na matiti makubwa na yalioyosimama vyema ni lazima utumie dawa hizi za matishamba ambapo mchanganyiko wake ndio umetoa fomula ya St Herb :
Fenugreek :
Kwa kawaida matunda ya mmea huu yalikuwa yanatumika na wanawake wa Kigiriki kuongeza ukubwa wa matiti yao na imehakikishwa kisayansi kuwa mtishamba huu huongeza athira ya mastogenic kwa misuli inayotengeneza maziwa.
matunda( mbegu ) ya mtuii huo yalikuwa yanatengeneza aina ya dawa ijulikanayo kama phytochemical diosgenin na estrogenic isoflavones zinazooongeza utengenezaji wa dawa ya estrogen katika mwili, dawa ambayo ni ufunguo kwa matiti yenye shepu ya mchonoko na yaliyojaa.
Mmea wa Saw Palmetto:Huu ni mmea wa kaskazini mwa Marekani na kwamba unafanana na mtende ni moja ya mmea wenye kemikali chache unaotengeneza musuli na husawazisha matatizo ya mkaziwa yenyewe.
Fennel Seed:Husaidia kuzalisha musuli nyingine mpya
L-Tyrosine:Hii ni amino acid, Tyrosine ambayo hudhibiti uzalishaji wa homoni na hivyo kupunguza unene na.
Mexican Wild Yam:Matumizi ya kila siku yanapunguza michirizi isiyotakiwa katika matiti.
Kelp:Ni zao la baharini. Ni chanzo bora cha madini ya iodine chakula chenye hiki huleta homoni zilizojipanga vyema.
Damiana:Kikawaida hutumika kwa ajili ya kuleta mizania ya homoni.Kuleta ukuzi mwema wa matiti, kupunguza dalili za matatizo yanayoambatana na siku za hedhi na kuchanganya ashiki;husaidia kupunguza uzito kuleta nguvu na kuondoa uchovu.
Dong Quai:kikawaida mmea huu wa Asia hutumika kuripea seli ikiwemo ya mammorianna, (tezi za matiti).
Mother's Wort:Mmea uliopo sehemu nyingi za Ulaya na kandoni mwa mito ambazo hutoa msukumo fulani katika kano la uzazi.
Black Cohosh :Mmea unaopatikana kaskazini mwa Marekani hutumika kama dawa ya kubadilisha homoni.
Avena Sativa:Ni kama shayiri na ina kiasi kikubwa cha saponins, flavonoids, minerals, na alkaloids kwa ajili ya mfumo wa homoni.
Humulus Lupulus:Husaidia kuimarisha matiti.
kisasili cha matiti
1. Kujiamini kwa mwanamke kumejikita zaidi katika ukubwa wa matiti yake
2. Wanawake hawana muwashawasha sana na ukubwa wamatiti yao
3. Brazia za kimichezo si za lazima.
4. matiti makubwa yanauhusiano na mambo ya ngono
5. Wanawake na matiti madogo hushindwa kunyonyesha kwa ufanisi
6. Wanawake wote hufurahia kutomaswatomaswa kwa matiti yao
7. Wanawake kwa kawaida huwa na matiti mawili yenye ukubwa unaofanana
8. Nywele kuzunguka chuchu huonyesha kwamba mwanamke huyu si wa kawaida
9. Wanawake na matiti makubwa ni wazazi sana
10.Unyonyeshaji husababisha matiti kuwa malapa
Alhamisi, 2 Julai 2015
On 01:58 by barbrawilliam in Afya No comments
Maambukizi ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa na uwepo wa fangasi wanaojulikana kitaalamu kama Candida albicans. Maambukizi haya pia hujulikana kama yeast infection au thrush. Fangasi hupatikana kama vimelea vya kawaida katika mdomo, mpira wa kupitisha chakula sehemu inayojulikana kama pharynx, katika kibofu cha mkojo, uume na hata kwenye uke.
Mfumo mzuri wa kinga wa mwili pamoja na aina fulani za bakteria wanaoishi pamoja na fangasi husaidia sana katika kuthibiti maambukizi yanayoyosababishwa na aina hi ya fangasi.
Kwa kawaida, Candida albicans huishi kwenye uke na sehemu nyingine kama zilivyoelezewa hapo juu bila kusababisha madhara yoyote yale isipokuwa pale mazingira ya eneo husika yanapobadilika kama vile mabadiliko katika hali ya PH ya eneo husika (ifahamike ya kwamba pH ya kawaida ndani ya uke ni 4.0 – 4.5) au uwiano wake na vimelea (microorganisms) lakini pia uharibiwa kutokana na sababu mbalimbali kama vile matumizi ya madawa aina ya antibiotics na kupungua kwa kinga mwilini kutokana na magonjwa mbalimbali n.k.
Maambukizi haya ya fangasi yanaweza kugawanywa katika sehemu kuu mbili;
- Maambukizi yasiyo makali yaani ‘uncomplicated thrush’ kwa kiingereza:
- Maambukizi makali yaani ‘complicated thrush’ kwa kiingereza:
Kwa kawaida Watu walio katika hatari ya kupata maambukizi ya fangasi hawa ni wale wenye;
- Kutumia sana dawa aina ya detergents kwenye sehemu za siri au douches (vifaa vinavyotumiwa kusafishia uke kwa kutumia maji yaliyochanganywa na jiki au antiseptic yoyote ile) kwa sababu hali hiyo husababisha kuharibika kwa uwiano wa fangasi na aina nyingine ya vinyemelezi kama bakteria aina ya lactobacilli
- Kutumia sana madawa aina ya antibiotics, steroids ambayo yana tabia ya kushusha kinga ya mwili
- Ugonjwa wa ukimwi (HIV/AIDS) n.k
ANGALIZO Wanawake wenye umri wa miaka kati ya ishirini na thelathini wapo kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi haya wakati wale ambao wameshaacha kupata hedhi au wale ambao hawajaanza kupata hedhi kabisa hawako kwenye hatari kubwa.
Dalili na viashiria kwa wanawake;
- Kuwashwa sehemu za siri (kwenye tupu ya mwanamke)
- Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri (burning sensation)
- Kufanya kama vidonda katika sehemu za siri (soreness)
- Maumivu wakati wa kujamiana (superficial dyspareunia)
- Maumivu au usumbufu wakati wa kujisaidia haja ndogo (wakati mtu anakojoa)
- Kuvimba na kuwa rangi nyekundu kwa mdomo wa nje wa tupu ya mwanamke (labia minora)
- Kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au nyeupe kijivu, unaoweza kuwa mwepesi, majimaji au mzito na ambao umefanana na jibini (cottage cheese like discharge) wenye muonekano unaojulikana pia kama curd-like appearance. Kwa kawaida, uchafu huu haumbatani na harufu yoyote isipokuwa panapokuwa na tatizo la ziada kama ugonjwa wa zinaa aina ya Bacteria vaginosis. Uchafu huu unaotoka hapa unaweza kuenea kwenye maeneo mengine yaliyokaribu na tupu ya mwanamke kama kwenye mitoki (groin area) au perineum na kusababisha kuharibika kwa ngozi katika sehemu hizo.
Dalili na viashiria hivi huwa mbaya zaidi wakati mwanamke anapokaribia kupata hedhi.
Dalili na viashiria kwa wanaume ni;
- Kuwashwa sehemu za siri
- Kuvimba na kuwa rangi nyekundu kwenye ncha ya uume
- Kuwepo kwa uchafu wa rangi nyeupe (kama nilivyoeleza hapo juu) kwenye sehemu ya juu ya uume.
- Kuwa na vidonda vidogo kwenye uume (sore on the glans)
Hata hivyo, mara nyingi wanaume hawaoneshi dalili zozote zile, ni vizuri kwa mwanamke kumueleza mwenza wake pale anapopata maambukizi haya ili naye pia apate kutibiwa.
Jumapili, 28 Juni 2015
On 01:16 by barbrawilliam in Afya No comments
1
Takribani asilimia 85 ya watu wenye harufu mbaya kinywani huwa na magonjwa ya kinywa na meno,Ikiwa harufu mbaya kinywani inasababishwa na magonjwa kinywani, dawa za kusafisha kinywa (mouthwash) haziwezi kuondoa tatizo zaidi ya kulifunika 
Magadi Soda:
Magadi soda ni mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Changanya kiasi kidogo cha magadi soda na maji ya kutosha kuunda kidonge kidogo na kisha weka au kandika kidonge icho sehemu ilio athirika na chunusi. Kwa muda wa dakika 15-20 au mpaka ikauke, na kisha suuza kwa maji yasiwe ya moto. Unaweza kurudia rudia mara kadhaa kwa siku mpaka utakapo ona athari ya chunusi imepotea.
Matango:
Unaweza kutumia Tango kwa kuondoa c
na hata kuondoa mabaka mabaka katika ngozi na kuifanya ngozi yako kuonekana yenye afya na yenye kuvutia.
mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Kata tango na kasha liponde ponde (unaweza kutumia blenda) kisha paka au kandika usoni. Wacha ikae kwa muda wa dakika 15-20 kisha suuza kwa maji baridi. Unaweza kurudia kwa siku mara mbili mpaka mara tatu kwa siku.
na hata kuondoa mabaka mabaka katika ngozi na kuifanya ngozi yako kuonekana yenye afya na yenye kuvutia.mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Kata tango na kasha liponde ponde (unaweza kutumia blenda) kisha paka au kandika usoni. Wacha ikae kwa muda wa dakika 15-20 kisha suuza kwa maji baridi. Unaweza kurudia kwa siku mara mbili mpaka mara tatu kwa siku.
Kitunguu Thaumu:
Unaweza kutumia kitunguu thaumu. Kuondoa chunusi. Matumizi ya Kitunguu thaumu, uleta matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na hata kuuwa bacteria sababu ina kemikali (antiseptiki) inayozuia kukua kwa bakteria kwenye jeraha au ngozi iliyo athirika kwa chunusi au hata kwenye kidonda. Na pia ina viwango vya juu wa salfa (ni zuri kwa ajili kukausha mafuta kwenye ngozi ya mwili). Twanga kitungu thaumu, au unaweza kukata nusu na kubandika sehemu iliyo na chunusi shikilia kwa dakika 5-10, na kisha safisha na maji baridi. Waweza kufanya ivyo asubuhi na jioni.
Mnana (Peppermint):
Unaweza kutumia majani ya Mnanaa kuondoa chunusi usoni.
Majani ya manna utumika hata kwa wale wenye matatizo ya Mba kwenye kichwa. Twanga majani machache au saga kisha weka sehemu iliyo athirika. Wacha mpaka pakauke na kisha safisha kwa maji baridi. Unaweza kufanya hivyo mara kadhaa kwa siku.
Majani ya manna utumika hata kwa wale wenye matatizo ya Mba kwenye kichwa. Twanga majani machache au saga kisha weka sehemu iliyo athirika. Wacha mpaka pakauke na kisha safisha kwa maji baridi. Unaweza kufanya hivyo mara kadhaa kwa siku.
Matumizi ya Limao:
Kata limao na kisha kwa kutumia kihenye pamba kiloweke kwa maji ya limao, sugua sehemu yenye chunusi, kisha wacha pakauke, unaweza kurudia rudi kila baada ya masaa kadhaa. Usitumie maji ya limao ya kwenye chupa, kwa sababu yameweka vihifadhi kemikali zingine kiasi cha kuondoa ubora wa kemikali halisi za kwenye limao. Tumia limao alisi.
Kutumia Asali:
Matumizi ya asali ni ya asili na ufanya ngozi, iwe na afya na nyororo. Kwa sababu kwenye asali kuna virutubisho vingi vyenye kazi ya kuua vimelea (bacteria) na kuzuia uchafu na kusinyaa kwa ngozi.
Weka asali kidogo sehemu ilio athirika na iwache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Vilevile unaweza kupaka uso mzima au hata mwili mzima ukitaka. Sababu asali inarutubisha ngozi ya mwili na kuifanya iwe na afya na mwonekano mzuri. Ukisha ridhika na muda wa asali kwenye ngozi yako unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya vuguvugu.
Weka asali kidogo sehemu ilio athirika na iwache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Vilevile unaweza kupaka uso mzima au hata mwili mzima ukitaka. Sababu asali inarutubisha ngozi ya mwili na kuifanya iwe na afya na mwonekano mzuri. Ukisha ridhika na muda wa asali kwenye ngozi yako unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya vuguvugu.
Kutumia Papai:
Unaweza kushangaa, lakini matumizi ya pa
ameonyesha matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na kusafisha sehemu zingine za mwili.
Ponda ponda kiasi kidogo cha papai na kisha iwache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Ukisha ridhika na muda unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya kawaida. Unaweza kurudia mara kadhaa kila siku kama unataka.
ameonyesha matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na kusafisha sehemu zingine za mwili.Ponda ponda kiasi kidogo cha papai na kisha iwache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Ukisha ridhika na muda unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya kawaida. Unaweza kurudia mara kadhaa kila siku kama unataka.
Dawa Ya Meno:
Unaweza kushaini ushangazwi na matokeo mazuri ya meno yako kusafishika kwa dawa ya meno.
Kemikali zinazotumika kuuwa Bakteria wa kwenye meno, pia zina uwezo wa kupambana na bakteria wengine. Tumia dawa ya meno isiyo na gel (non-gel) paka kwenye chunusi. Ni vizuri ukatumia usiku wakati wa kwenda kulala, ila si vibaya ukipaka hata muda wa asubuhi au mchana mradi tu uwe na muda wa kutosha wa dawa kukauka ili iweze kufanyakazi vizuri.
Namna nyingine ni kuchanganya dawa ya meno na unga wa mahindi au nganoiuliosagwa na kuwa laini sana. Unaweza kupaka na kuiwacha ikauke kwa dakika tano mpaka 10.
Safisha kwa sabuni. Mchanganyiko huu unasaidia kukausha chunusi.
Kemikali zinazotumika kuuwa Bakteria wa kwenye meno, pia zina uwezo wa kupambana na bakteria wengine. Tumia dawa ya meno isiyo na gel (non-gel) paka kwenye chunusi. Ni vizuri ukatumia usiku wakati wa kwenda kulala, ila si vibaya ukipaka hata muda wa asubuhi au mchana mradi tu uwe na muda wa kutosha wa dawa kukauka ili iweze kufanyakazi vizuri.
Namna nyingine ni kuchanganya dawa ya meno na unga wa mahindi au nganoiuliosagwa na kuwa laini sana. Unaweza kupaka na kuiwacha ikauke kwa dakika tano mpaka 10.
Matumizi ya Poda:
Matumizi ya Mvuke:
Unaweza kutumia mvuke (Steam/vapour) kuondoa mafuta yaliozidi kwenye ngozi ya uso wako. Kwa kujifukisha. Kwa wale ambao hawana mashine wanaweza kujaza sufuria au bakuli kwa maji ya moto na kujifunika kwa taulo uku ukielekeza uso wao kwenye sufuria au bakuli lenye maji yanayotoa mvuke k wa dakika 5-10. Unaweza kufanya hivi pamoja na njia mojawapo nilizo zitaja hapo juu.
Tahadhari:
Njia hizi za Asili, uchukuwa muda kidogo mpaka kuona matoke ya kuridhisha.
Njia zote hizi kama hazijaleta matokeo mazuri, tafadhali muone daktari wa ngozi au nenda hospitali ilio karibu kwa uchunguzi zaidi wa ngozi yako.
Njia zote hizi kama hazijaleta matokeo mazuri, tafadhali muone daktari wa ngozi au nenda hospitali ilio karibu kwa uchunguzi zaidi wa ngozi yako.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)
Search
Popular Posts
-
Faida za kutumia ua la Ulimi wa Mama Mkwe kiroho ni nyingi sana, hasa kwa mtu mwenye macho ya rohoni au anayejishughulisha na mambo ya kinga...
-
ALLY REHMTULAH KUJA NA UFAHARI WETU FESTIVAL Mbunifu wa mavazi nchini Tanzania Allyrehmtullah ameandaa tamasha linalokwenda kwa jina ...
-
JACKSON KABIRIGI'S PROFILE
-
UREMBO ni jambo muhimu kwa mwanamke kwa kujiweka nadhifu wakati wote ikiwa ni pamoja na kujipamba na kujifanyia usafi wa mwili. Watu wengi w...
-
Fainali ilikua ni Jumamosi ya April 18 2015 ambapo shindano la Airtel Trace Music Stars lilifanyika Nairobi Kenya likiwa ni shindano ...
-
Msanii Linah Sanga alimaarufu kama Ndege mnana amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye nje ya kazi yake ya sanaa ni msusi mzuri wa nywele na al...
-
urembo Fashionable lineup ... Rihanna, Beyonce, Jay Z, Kim Kardashian, Jennifer Lopez and Sarah Jessica Parker. Pictures: Getty Source...
-
Magadi Soda: Magadi soda ni mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Changanya kiasi kidogo cha magadi so...









