Ijumaa, 26 Juni 2015

On 08:08 by barbrawilliam in , ,    No comments
UREMBO ni jambo muhimu kwa mwanamke kwa kujiweka nadhifu wakati wote ikiwa ni pamoja na kujipamba na kujifanyia usafi wa mwili. Watu wengi wamekuwa na uelewa mdogo juu ya masuala ya urembo kwa kudhani kuwa urembo ni kujipaka poda tu usoni na wanja kwenye nyusi huku wakisahau kuwa urembo ni pamoja na kuufanya usafi mwili kwa ujumla
Kwani huwezi kupaka poda kama sura yako si safi.Leo katika safu hii utaona jinsi gani unaweza kubandika kucha za bandi kama una kucha fupi. Kabla ya kubandika kucho hizi hakikisha kucha zako za zsili zinakuwa safi kwa kuziosha na kuzitoa uchafu uliopo ndani ya kucha ili ziweze kuwa safi na kuweza kubandika kucha.
Baada ya kucha hizo kuwa safi unaweza kubandika hizo kucha za bandia bilakusahau kuhakikisha zote zinakuwa katika usawa mmoja tayari kwa ajiri ya kupaka rangi uipendayo. Lakini kumbuka wataaramu wanashauri kucha za bandia zisikae kwa muda mrefu bila kutolewa kwani zinaweza kusababisha kucha halisi kuoza, hivyo wanashauri zitolewe baada ya wiki mbili na si zaidi.

Lakini pia wanashauri kutumia dawa maalumu ya kutolea na si kutoa kienyeji kwani zinaweza kukusababishia maumivu pamoja na kuzifanya kucha halisi kuwa na muonekano mbaya wa mabonde mabonde

0 maoni:

Chapisha Maoni