Jumapili, 28 Juni 2015

On 01:49 by barbrawilliam in ,    No comments
Msanii wa filamu nchini ambaye pia ni Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu, kufungua duka kubwa la urembo nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa chanzo cha karibu nchini humo, Wema Sepetu aliongozana na dada yake baada ya kuwa kwenye mazungumzo ya muda mrefu na kampuni inayotaka kufanya kazi na Wema Sepetu pamoja kusambaza filamu yake ya D.A.D aliyocheza Na msanii maarufu kutoka Ghana Van Vicker, filamu hiyo inayotarajiwa kuoneshwa kwenye kumbi mbali mbali za sinema pamoja na kusambazwa Afrika Kusini. Pamoja na wao kusambaza pia kampuni ya Endless Fame Production kutoka Tanzania pamoja na kampuni ya Sky and Orange production ya Ghana wamejiandaa vilivyo kuhakikisha filamu hiyo inapenya kimataifa tayari USA, UK, Canada na nchi nyinginezo karibuni wataachia website watu kufanya pre-order ya filamu ya D.A.D.

Mmoja wa wenyeji wa Wema Sepetu nchini Afrika Kusini ambaye wamepiga picha nyingi za matangazo ya biashara hiyo ya vipodozi vyenye jina la Wema Sepetu, ameonekana pia nchini wakifanya vikao na wadau mbali mbali jinsi gani ya kufanya biashara kimataifa ambapo tayari mbali na Nigeria, kituo kingine kitakuwa Zimbabwe. Katika hali iliyopokelewa vyema nalo kundi maarufu Uganda na Afrika Kusini Rich Gang la Mume wa ZARI wako tayari kumsapoti na kutangaza duka jipya la Wema Sepetu litakaloanzishwa Afrika Kusini litakalouza vipodozi mbali mbali, pia litakua ni moja ya kituo cha kusambaza na kununua filamu za EndlessFame ambazo zitaachiliwa.

Nagar alisema Wema ni binti mwenye kipaji cha kuigiza pia ni mrembo haitoshi kujulikana Tanzania pekee bali na nje ya Tanzania ambapo tayari Wema na baadhi ya watu wa karibu yake wamekua wakienda Afrika Kusini mara kwa mara kuangalia mahali sahihi kuwekeza nchini humo.

Kwasasa Wema Sepetu amekuwa busy kufanya filamu mbali mbali nchini lakini pia kwenye maandalizi ya kuzindua movie yake ya DAD mwaka huu. Amewataka mashabiki wake kuvumilia maana anafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha hawaangushi na watafurahia. Baada ya mwezi Ramadan tutaona suprise nyingine ambazo uongozi wake wanasubiri kutoa tamko kuhusu mwonekano mpya wa Wema Sepetu. Mpaka sasa haijajulikana ni aina gani ya vipodozi vitakavyokua na jina la msanii Wema Sepetu. #BeWemaFanyaWema

0 maoni:

Chapisha Maoni