Ijumaa, 26 Juni 2015

On 04:32 by barbrawilliam in ,    No comments
Hili ni jambo ambalo wamekuwa wakilipenda watu wengi lakini hujikuta kwenye wakati mgumu hasa linapokuja suala la uchaguzi wa mavazi hayo. 

Umewahi kutamani kuwa na mwonekano wa kimavazi unaoendana na mwenza wako na hujui ufanye nini?

Hili ni jambo ambalo wamekuwa wakilipenda watu wengi lakini hujikuta kwenye wakati mgumu hasa linapokuja suala la uchaguzi wa mavazi hayo. 

Ugumu huu utokea mara nyingi katika kupata nguo ambayo inaweza kuvaliwa na mwanamke na mwanaume bila kuleta muonekano wa ajabu.

Zamani hili lilikuwa likiwezekana kwa urahisi kwa kutumia vitenge lakini siku hizi jambo hili limekuwa likiwezekana kutokana na kuwapo nakshi za kila aina kwenye mitindo. 

Wabunifu wa masuala ya urembo wanasema unaweza kutumia aina yoyote ya mavazi na kushona kwa mtindo muutakao.

Sambamba hilo pia mnaweza kutumia rangi za aina moja wakati mnachagua mavazi yenu. 

Kuvaa nguo zinazofanana na mpenzi wako haijalishi ni sehemu muhimu kama katika dhifa mbalimbali bali pia mnaweza kuwa na kawaida ya kuvaa mavazi hayo katika mitoko yenu ya kawaida kama ofisini, mnapokuwa katika matembezi katika fukwe za bahari pia hata mnapoenda kufanya ununuzi wa bidhaa zenu za nyumbani.

Mnaweza kuvaa suruali za jeans na tisheti au mashati yanayofanana lakini pia mnaweza kushona nguo ambazo zitakuwa na nakshi ya kitenge au khanga na wote mkaonekana mmeng’ara. 

Bazee pia linaweza kushonwa nguo za jinsi zote na kuleta mwonekano mzuri kwa wavaaji mnapoongozana pamoja.

Mnaweza pia kuchagua nguo za rangi zinazofanana hata kama zitakuwa katika mitindo tofauti lakini bado mtaonekana mmependeza. Hapa mwanamke anaweza kuvalia nguo yake yoyote na ili kwenda sambamba na mwenzi wake basi ataangalia moja ya rangi zilizopo katika gauni hilo na yeye akavaa shati na wote wakaonekana wanapendeza.

Wakati mwingine si lazima kuvaa nguo zinazofanana bali pia mwanaume anaweza kutumia tai yenye rangi zinazofananana nguo ya mwenzi wake. Hapa anaweza kuvaa tai ndevu au fupi ili mradi iwe na rangi ambazo zipo katika nguo ya mwezi wake.

Kwa kufanya hivyo muda wote wewe na mpenzi wako mtaonekana mnapendeza na kuvutia machoni kwa watu.

0 maoni:

Chapisha Maoni