Ijumaa, 21 Agosti 2015

On 00:18 by barbrawilliam in , ,    No comments
KAA UKITAMBUA KUWA MKE NI MATUNZO, YAANI SAWA NA MGOMBA KUPALILIWA KILA WAKATI!!! Assalaam alaikum/Bwana Yesu asifiwe! Bila shaka mna afya njema wasomaji wangu. Kikubwa mjue naendelea kuwapenda, kuwathamini na kuwaheshimu kwani mmekuwa mkionesha kukubali kile ambacho nakiandika kupitia safu hii.

Ndiyo maana leo nimeamua kuwasema wanaume kwa sababu nao ni miongoni mwa watu ambao hawajakamilika na wanastahili kukumbushwa baadhi ya mambo ili ndoa zao ziwe tamu, au siyo jamani?
Ujumbe mwingi ninaopokea kutoka kwa wanaume umenifanya nigundue kuwa wengi wenu mna kasoro na mnatakiwa kuzifanyia kazi ili kulinda ndoa zenu.
Hivi mnafahamu kitu muhimu kwa mwanamke ni suala la kuhakikisha amekula, amepata nguo nzuri na burudani faragha?

Wengi wa wanaume hawalijui hilo kabisa kwani wanadhani mwanamke akishapewa burudani ya ndoa inatosha, wanasahau kuwa kuna umuhimu wa kuhakikisha anapendeza na anakula vizuri pia.

Kuna wanaume kazi yao kuwasifia wake za watu bila kujua kuwa hata mkeo ukimjali atakuwa na mvuto na atasifiwa. Yaani mkeo tangu umemm-nunulia nguo ya harusi ndiyo imetoka, hata siku moja hujawahi kumnunulia hata leso, hujawahi kumpa ‘kijihela’ angalau akanunue nguo.
Huna mawazo ya kumpa hata pesa akanunulie ‘vijiurembo’ ili angalau akipita mbele za watu aonekane ni mke wa mtu anayethaminiwa. Hilo ni tatizo kwenu wanaume.Matunzo hamtoi inavyotakiwa, tena wengine wanajiangalia wao tu. Hivi unajisikiaje pale unapojipendezesha wewe tu wakati mkeo anaonekana yupo yupo tu? Badilikeni jamani, tena nasisitiza mbadilike!

Nimetoleo mfano mgomba kwamba unastahili kupaliliwa na kumwagilia ili uweze kukua vizuri. Vivyo hivyo kwa mkeo. Ili aonekane amependeza, hilo jukumu unalo wewe mume! Usitarajie eti kwa kuwa anajishugulisha basi ajipendezeshe mwenyewe, hiyo ni sawa kweli?
Hatukatai mke kujinunulia nguo, urembo na vitu vingine lakini je kama hana uwezo wa kufanya hivyo afanyeje? Wewe ulipoamua kumuoa si ulijiaminisha kwamba utaweza kumtunza? Sasa mbona humjali na kumtuza ipasavyo?

0 maoni:

Chapisha Maoni