Jumatatu, 10 Aprili 2023

On 02:36 by barbrawilliam   No comments

Jumanne, 21 Machi 2023

On 07:10 by barbrawilliam   No comments
washiriki wa mkutano wa kujadili masuala ya matumizi ya Nishati safi na salama kwenye Magari mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo Machi 21, 2023. WADU wa Usafiri kutoka nchi 17 za Kikanda Afrika wajadili masuala ya matumizi ya Nishati safi na salama kwenye Magari hapa nchini jijini Dar es Salaam leo Machi 21, 2023. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akimwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Angela Kairuki akizungumza wakati wa kufungua kikao kazi hicho amesema kikao kazi hicho kitajadili masuala ya matumizi ya umeme kwenye magari pamoja na matumizi ya betri ili kuepukana na uchafunzi wa mazingira na hali ya hewa. Amesema magari yanayotumia umeme yatasaidia katika utunzaji wa mazingira na kuzuia uharibifu wa hali ya hewa ili kuendana na sera ya dunia inavyopambana na kukabiliana na uchafuzi wa mazingira. Kwa upande wa Afya amesema kuwa Usafiri huo utaoanzia jijini Dar es Salaam utapunguza jamii kupata matatizo ya afya yanayotokana na uchafunzi wa hali ya hewa pamoja na kupunguza gharama za matibabu ya maradhi mbalimbali hasa yanayosababishwa na uchafuzi wa hali ya hewa. Kwa Upande wa teknolojia ameeleza kuwa jamii inatakiwa kuwa na uelewa thabiti katika matumizi ya magari ya umeme ambapo kutatakiwa kuwe na muendelezo wa miundombinu pamoja na kuachana teknolojia ya kutumia mafuta ya magari. "Hii ni mhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania pamoja na kupunguza gharama kwa utumiaji magari ya Umeme." Magari ya usafiri wa umma yanawajibika na unachangia asilimia 67.4 ya uchagunzi mazingira unaotokana na hewa ukaa. Akizungumzia kuhusiana na mradi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Makalla amesema kuwa kunafaida kubwa za kujenga miundombinu jijini Dar es Salaam kwa sababu inasaidia wananchi kupata usafiri wa uhakika na kubeba watu wengi kwa wakati mmoja. Amesema kuwa sekta ya usafiri inachangia kuleta uharibifu wa mazingira unaotokana na hewa ya Kabonidayoksaidi. Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Dkt. Edwin Mhede amesema kuwa katika Mjadala watajadili namna nchi za Afrika zinaweza kuja na matumizi ya magari yanayotumia nishati rafiki ili kupunguza kiwango cha hewa ya ukaa ambayo huzalishwa kila uchwao kutoka kwenye magari yanayotumia nishati ya mafuta. Amesema mkutano huo unalenga kujadili kubadili matumizi ya mabasi au magari yanayotumia nishati ya umeme katika majiji yanayoendelea katika nchi za kikanda za Afrika. Amesema nishati ya umeme inatoa kiwango cha kabonidayoksaidi kwa kiwango cha sifuri kwasababu kunakuwa hakuna makelele wala uchafunzi wa hali ya hewa. Akizungumzia kuhusiana na Changamoto zilizopo amesema kuwa uelewa wa jamii ni mdogo na Kila jambo linaeleweka kwa kujifunza na kupeana elimu, pia amesema kuanachangamoto za kimuundo ambapo changamoto hizo zinahitaji sera za uhakika, kama sera za kisheria, za kikodi na sera za uwekezaji, sera za fedha. "Mazingira hayo lazima yafungamanishwe yote ili kutoa motisha ya wawekezaji ambao wanaweza kuwekeza kwenye sekta ya uzalishaji wa magari au watakao agiza magari kutoka nje ya nchi kule nchini kwaajili ya kutoa huduma. Hata kwa Sisi waendeshaji tunahitaji kupata mazingira wezeshi ya kisera, ambayo yatapelekea kuona thamani ya fedha iliyowekezwa." Amesema Dkt. Mhede Akizungumzia mradi wa BRT Dkt. Mhede amesema kuwa mtaji mkubwa uliopo Dar es Salaam ni miundombinu kukua kwa kasi na 'icon' Nembo ya BRT Afrika amesema ipo Dar es Salaam pia kwasiku moja wanahudumia watu zaidi ya laki mb
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akizungumza wakati wa kufunguzi kikao kazi cha washiriki kutoka nchi 17 wakijadili masuala mbalimbali ya matumizi nishati safi katika magari. Kikao kazi hicho kimefunguliwa leo Machi 21, 2023 jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Dkt. Edwin Mhede, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kufunguliwa kwa kikao kazi cha wawakilishi kutoka nchi 17 za kanda ya Afrika wa kujadili masuala ya matumizi ya Nishati safi na salama kwenye Maga
Picha ya pamoja
Mwakilishi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Rwanda, Janvier Twagirimana akizungumza wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya matumizi ya Nishati safi na salama kwenye Magari. Pia ameelezea namna usafiri nchini Rwanda unavyofanya kazi ikiwa ni pamoja kutumia Baiskeli zinazotumia umeme
On 06:54 by barbrawilliam   No comments
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Komred Abdulrahman Kinana afungua Mafunzo ya Umoja wa wanawake wa Tanzania (UWT) kwa Wajumbe wa Baraza kuu ,Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa na Wilaya katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma. *WAELEZENI MAZURI YALIYOFANYWA NA RAIS Dk. SAMIA KUTEKELEZA ILANI YA CCM: KINANA* MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amewataka viongozi wa CCM wayaeleze kwa wananchi mambo mazuri yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. Kinana aliyasema hayo jijini hapa jana, wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kuanzia ngazi ya Taifa hadi Wilaya. “Katika maeneo yenu hakikisheni mnakisemea Chama na mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia, wala msione haya kusema ili wananchi wajue na hata katika chaguzi zijazo tusipate shida. Alisisitiza kuwa: "Chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia katika kipindi cha miaka miwili kila kata kuna alama ya maendeleo kuanzia shule, zahanati, barabara na maendeleo ya watu, tuna kila sababu ya kujisifia na kuusifia uongozi wa mwenyekiti wa chama hiki." Vilevile, Kinana aliwataka viongozi wa UWT kubeba ajenda za wanawake kitaifa bila kuogopa jambo lolote.
KUHUSU UCHAGUZI Akizungumzia kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, Kinana aliwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ili kufia lengo la kujenga jamii yenye usawa. Alisema mwakani kuna uchaguzi wa viongozi wa serikai za mitaa, hivyo ni vyema wanawake wakajitokeza kuchukua fomu kuomba nafasi mbalimbali za uongozi na CCM itawapa ushirikiano wa kutosha. “Kuelekea uchaguzi ujao jiandaeni na kuwahimiza wanawake kuwania nafasi zote za uongozi na ninawahakikishia kuwa, CCM itawaunga mkono kwa hali na mali ili kuwa na wanawake wengi waliochaguliwa katika majimbo,”alisema.
ASISITIZA VIKAO Katika hatua nyingine, Kinana aliwataka UWT kuhakikisha maamuzi mengi yanafanyika kupitia vikao na sio maamuzi ya mtu mmoja au kikundi cha watu. Alisisitiza kuwa hata kiongozi anapokosea sio busara kumuamisha kituo cha kazi kabla ya kumuita na kumsikiliza kwani utakuwa ni ukiukwaji wa haki. “Niwasihi tumieni vikao kuamua mambo sio kikundi cha watu, kila kitu lazima kijadiliwe kwa kina na kipite kwa hoja kwa sababu ndani ya CCM hakuna maamuzi ya mtu mmoja au amri, ninyi katika maeneo yenu hakikisheni ndani ya vikao huko ndio haki ya mtu itapatikana. “Wenyeviti mpunguze kuhamisha watu hovyo, kama mtu amekosea aitwe aelezwe kosa sio kuchukua maamuzi ya haraka una muhalibia mtu mwelekeo, tujenge utamaduni wa kuambiana ukweli na msiogopane mtu anapokosea,”alisema. Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM aliwashauri viongozi kusoma vitabu mbaimbali vya Chama ikiweo Ilani ya uchaguzi, sera, kanuni na katiba kwani vitawasaidia katika masuala mbalimbali ya uongozi. Alisema CCM ni miongoni mwa vyama vichache duniani ambayo vinamaandishi mengi. “Someni katiba, kanuni, ilani na sera kwani vitawasaidia kuendesha shughuli mbalimbali za Chama na kuongoza kwa kuzingatia misingi ya haki,”alisema
UWT WAELEZA Awali, Mwenyekiti wa UWT Taifa, Marry Chatanda, alisema wanawake wanaridhika na kazi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia kwani ilani ya CCM inatekelezwa kwa kishindo. Alisema katika kipindi cha miaka miwili ya serikali ya awamu ya sita hakuna kilichosimama ndio maana waliandaa hafla ya kumpongeza Rais Dk.Samia kwa kazi nzuri alizozifanya. “Sisi wanawake wa CCM hakika tumeridhishwa na uongozi wa Rais Dk.Samia na tunaahidi katika uchaguzi wa mwaka 2025 tutatoa fedha kwa ajili ya kumchukulia fomu mwanamke mwenzetu,”alisema. Kwa upande wake, Katibu wa UWT Taifa Dk. Philis Nyimbi alisema lengo la mafunzo hayo ni kuleta ustawi na kuwapatia viongozi maarifa namna ya kuongoza jumuiya hiyo katika ngazi zote. Alisema mafunzo hayo yamewakutanisha viongozi 478 ambapo baada ya kumaliza elimu waliyoipata wataipeleka katika ngazi ya kata na matawi. “Mafunzo haya ni mahususi kwa ajili ya kuwajengea uwezo viongozi wetu ukizingatia tunaelekea katika uchaguzi mkuu mwaka 2025, hivyo kutokana na mafunzo haya watatakiwa kuyapeleka katika ngazi ya kata na matawi na kutuletea taarifa,”alifafanua.
On 06:29 by barbrawilliam in    No comments
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema kuwa Bandari Kavu ya Kwala inatarajiwa kuanza kufanya kazi muda wowote kuanzia sasa na itatoa huduma zote za kiforodha kama zinavyotolewa katika Bandari zingine. Akizungumza hivi karibuni kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa, Meneja Miliki wa Mamlaka hiyo, Alexander Ndibalema ameeleza kuwa, kukamilika kwa bandari hiyo ni matokeo chanya ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita ambayo imewezesha takriban Shilingi bilioni 83.247 kutumika katika kuendeleza bandari, ujenzi wa barabara ya zege yenye urefu wa kilometa 15.5 kutoka barabara kuu ya Morogoro eneo la Vigwaza kuelekea bandarini na kusogeza miundombinu ya reli mchepuko yenye urefu wa kilometa 1.3.
"Bandari Kavu ya Kwala ipo tayari kufanya kazi kwa sababu miundombinu yote ya msingi imekamilika na leseni zingine kutoka mamlaka zingine za Serikali zimeshakamilika ambapo kinachosubiriwa kwa sasa ni kupata leseni kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)", alisema Ndibalema. Ndibalema ameongeza kuwa, lengo kuu la kuanzisha bandari hiyo ni kuongeza ufanisi na kiasi cha shehena inayohudumiwa katika bandari ya Dar es Salaam, kupunguza msongamano katika bandari ya Dar es Salaam, kuongeza mapato ya Serikali kupitia huduma zitolewazo katika Bandari. Hivyo wateja kutoka sehemu mbalimbali wataweza kuchukulia mizigo yao ndani ya bandari hiyo ambayo ina uwezo wa kuhudumia wastani wa makasha 823 kwa siku sawa na makasha 300,395 kwa mwaka sawa na asilimia 30 ya makasha yote yanayohudumiwa katika Bandari ya Dar es Salaam kwa sasa.
Vile vile amefafanua kuwa, bandari hiyo ni ya kimkakati kwa sababu eneo la Kwala lina miradi mingi ya kimkakati ambayo imeanza kutekelezwa ikiwemo ujenzi wa viwanda mbalimbali na ujenzi wa Mji mpya wa Kwala, hivyo ni matarajio kuwa mizigo ya Wawekezaji kutoka nchi mbalimbali inayokwenda kwenye viwanda itachukuliwa hapo. Ameeleza kuwa, bandari hiyo inatarajiwa kuchangia kwa kiwango kikubwa katika Pato la Taifa ambapo sehemu kubwa ya mizigo itakayohudumiwa katika bandari hiyo ni ile inayokwenda nchi jirani. Bandari hiyo imejengwa kwa awamu mbili zilizojumuisha usafishaji wa eneo lenye ukubwa wa Hekta 60 na ujenzi wa ukuta uliogharimu Shilingi 9,465,643,798.00, ujenzi wa Yadi hekta 5 kiwango cha zege uliogharimu Shilingi 36,670,971,842.00, ujenzi wa Reli Mchepuko yenye urefu wa KM 1.3 uliogharimu Shilingi 677,328,320.00 na ujenzi wa barabara yenye urefu wa KM 15.5 kwa kiwango cha zege uliogharimu Shilingi 36,432,867,115.70 ambayo imekamilika kwa asilimia 100.

Alhamisi, 2 Februari 2023

On 08:27 by barbrawilliam   No comments
Katika kuadhimisha miaka 46 ya chama Cha mapinduzi wanachama wa UWT Turiani wilaya ya mvomero wameshiriki upandaji wa miti karibu na mto mbulumi uliopo tarafa ya Turiani wilaya ya Mvomero ili kusaidia kuzuia madhara yanayotokana na kufurika kwa mto huo kipindi Cha mvua
Sambamba na hilo mwenyekiti wa UWT ambaye pia ni mgeni rasmi wa maadhimisho hayo ndugu Rachel Steven Kingu ameongoza ugawaji wa vifaa mbalimbali vya usafi katika zahanati ya Turiani wilaya ya Mvomero ikiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha vituo vya afya nchini. Aidha ndugu Kingu ameshiriki zoezi la ugawaji wa kadi za Chama Cha Mapinduzi kwa wanachama wapya na kutoa hamasa kwa viongozi wa ngazi zote hasa madiwani kushirikiana na serikali katika kufanikisha adhma ya chama na serikali kwa ujumla
On 04:43 by barbrawilliam   No comments
On 04:42 by barbrawilliam   No comments
On 04:38 by barbrawilliam   No comments
On 04:23 by barbrawilliam   No comments

Jumatano, 1 Februari 2023

On 22:29 by barbrawilliam   No comments
On 21:14 by barbrawilliam   No comments
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kufanya uchunguzi wa bili na bei za maji kwa wananchi wilayani Malinyi mkoani Morogoro ili kupata ukweli iwapo wananchi hao wanabambikiwa bili au lah. Kauli hiyo ameitoa leo katika Kata ya Mtimbila aliposimamishwa na wananchi akiwa katika msafara wake kuelekea Makao Makuu ya Wilaya ya Malinyi kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kama ilivyoahidiwa kwenye Ilani ya CCM. Mara baada ya kusimamishwa eneo hilo na wananchi walitoa kero yao kuwa bili ya maji ni sambamba na gharama za kununua maji ambapo pamoja na kwamba chanzo cha maji ni cha mserereko lakini bado wanatozwa shilingi 100 kwa ndoo ya lita 20. Aidha,wamema bei ya maji wanayotozwa kwa mwezi kwa wale ambao hawajafungiwa mita za maji za ni shilingi 7,000 na bili hiyo inalipwa kila mwezi hata kama maji hayatoki. Akijibu kero hiyo ambayo pia imetolewa na wananchi katika Wilaya ya Kilombero,Chongolo aliagiza Takukuru kufanya uchunguzi ili kuona uhalali wa bei hizo kwani mwongozo wa malipo ya maji ya chanzo hicho ni shilingi 20, kwa ndoo moja ya maji ya lita 20. “Takukuru,hili lichukueni lichunguzeni kuona uhalali wake,maana nimepewa kero hii mara nyingi,sasa lifanyieni kazi,”amesema Chongolo. Chongolo yupo katika ziara ya kikazi mkoani Morogoro akiwa ameongozana na Katibu wa Halmashauri Kuuya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema na Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Haji(Gavu)