Jumatano, 1 Februari 2023
On 21:14 by barbrawilliam No comments
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kufanya uchunguzi wa bili na bei za maji kwa wananchi wilayani Malinyi mkoani Morogoro ili kupata ukweli iwapo wananchi hao wanabambikiwa bili au lah.
Kauli hiyo ameitoa leo katika Kata ya Mtimbila aliposimamishwa na wananchi akiwa katika msafara wake kuelekea Makao Makuu ya Wilaya ya Malinyi kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kama ilivyoahidiwa kwenye Ilani ya CCM.
Mara baada ya kusimamishwa eneo hilo na wananchi walitoa kero yao kuwa bili ya maji ni sambamba na gharama za kununua maji ambapo pamoja na kwamba chanzo cha maji ni cha mserereko lakini bado wanatozwa shilingi 100 kwa ndoo ya lita 20.
Aidha,wamema bei ya maji wanayotozwa kwa mwezi kwa wale ambao hawajafungiwa mita za maji za ni shilingi 7,000 na bili hiyo inalipwa kila mwezi hata kama maji hayatoki.
Akijibu kero hiyo ambayo pia imetolewa na wananchi katika Wilaya ya Kilombero,Chongolo aliagiza Takukuru kufanya uchunguzi ili kuona uhalali wa bei hizo kwani mwongozo wa malipo ya maji ya chanzo hicho ni shilingi 20, kwa ndoo moja ya maji ya lita 20.
“Takukuru,hili lichukueni lichunguzeni kuona uhalali wake,maana nimepewa kero hii mara nyingi,sasa lifanyieni kazi,”amesema Chongolo.
Chongolo yupo katika ziara ya kikazi mkoani Morogoro akiwa ameongozana na Katibu wa Halmashauri Kuuya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema na Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Haji(Gavu)
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Search
Popular Posts
-
ALLY REHMTULAH KUJA NA UFAHARI WETU FESTIVAL Mbunifu wa mavazi nchini Tanzania Allyrehmtullah ameandaa tamasha linalokwenda kwa jina ...
-
Faida za kutumia ua la Ulimi wa Mama Mkwe kiroho ni nyingi sana, hasa kwa mtu mwenye macho ya rohoni au anayejishughulisha na mambo ya kinga...
-
UREMBO ni jambo muhimu kwa mwanamke kwa kujiweka nadhifu wakati wote ikiwa ni pamoja na kujipamba na kujifanyia usafi wa mwili. Watu wengi w...
-
JACKSON KABIRIGI'S PROFILE
-
Rangi ya mdomo ni moja ya vipodozi vinavyoongeza urembo kwa mwanamke.Kuna rangi mbalimbali za mdomo kulingana na anachopenda kupaka mrembo h...
-
Asilimia kubwa ya watu wamekuwa na tatizo la kuwa na makovu yanayosababishwa na chunusi kwa kipindi kirefu bila kupata ufumbuzi, na hii ...
-
MISS KINONDONI 2019 PRESS BONANZA Leo miss kinondoni wamefanya special bonanza kwa lengo la kuchangia kituo ch...
-
Tanzania ni moja ya nchi zilizoko chini ya jangwa la sahara afrika imekuwa na wimbi la kuongezeka kwa watu wenye ulemavu ngozi ,jamii y...
Recent Posts
Categories
Sample Text
Blog Archive
-
▼
2023
(11)
-
▼
Februari
(7)
- UWT TULIANI WAFANYA MAAJABU KUADHIMISHA MIAKA 46 Y...
- SENETA SANGA "MLIAHIDI KUJENGA UWANJA DODOMA, UKO ...
- WAKINA BABA NAO WAKOPESHWE MBUNGE AWAKA
- Luhaga Mpina Ashangazwa na Majibu ya Waziri wa Fed...
- Waziri Mkuu Serikali Haitafumbia Macho Adhabu Shu...
- MH RAIS SAMIA AZINDUA TUME YA KUANGALIA JINSI YA ...
- CHONGOLO AIAGIZA TAKUKURU KUCHUNGUZA BILI ZA MAJI ...
-
▼
Februari
(7)





0 maoni:
Chapisha Maoni