Alhamisi, 2 Februari 2023

On 08:27 by barbrawilliam   No comments
Katika kuadhimisha miaka 46 ya chama Cha mapinduzi wanachama wa UWT Turiani wilaya ya mvomero wameshiriki upandaji wa miti karibu na mto mbulumi uliopo tarafa ya Turiani wilaya ya Mvomero ili kusaidia kuzuia madhara yanayotokana na kufurika kwa mto huo kipindi Cha mvua
Sambamba na hilo mwenyekiti wa UWT ambaye pia ni mgeni rasmi wa maadhimisho hayo ndugu Rachel Steven Kingu ameongoza ugawaji wa vifaa mbalimbali vya usafi katika zahanati ya Turiani wilaya ya Mvomero ikiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha vituo vya afya nchini. Aidha ndugu Kingu ameshiriki zoezi la ugawaji wa kadi za Chama Cha Mapinduzi kwa wanachama wapya na kutoa hamasa kwa viongozi wa ngazi zote hasa madiwani kushirikiana na serikali katika kufanikisha adhma ya chama na serikali kwa ujumla

0 maoni:

Chapisha Maoni