Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Udaku. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Udaku. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 5 Mei 2015

On 07:23 by barbrawilliam in ,    No comments


barbra william
Hatari sana! Mkali wa Ngoma ya Chekecha Cheketua, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ amenusurika kifo baada ya kuvamiwa nyumbani kwake na majambazi ambao walimteka mlinzi na ndugu yake mmoja kisha kuwashushia kibano kikali huku wakiwaamuru wawapeleke kwenye chumba anacholala msanii huyo,
Mlango nyumbani kwa Alikiba ukionekana jinsi ulivyovunjwa na majambazi na kuiba vitu.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa na mwandishi wetu Mei 2, mwaka huu, Abdul Kiba ambaye ni mdogo wa Ali Kiba, alisema usiku wa siku ya tukio alipewa taarifa na Ali Kiba kuwa amevamiwa na majambazi wenye silaha za moto hivyo alikurupuka moja kwa moja hadi Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar ambapo waliripoti na baadaye kupata msaada wa polisi hadi eneo la tukio nyumbani kwa jamaa huyo Kunduchi Beach.

Sebuleni kwa Alikiba vitu vikiwa vimezaga zagaa baada ya kuvamiwa na majambazi na kuibiwa.
“Wakati linatokea tukio hilo nilikuwa Masaki (Dar) na jamaa yangu mmoja anaitwa Bude, kaka (Ali) alinipigia simu na kuniambia kilichotokea nasi hatukuchelewa tukaenda polisi na kuwaeleza hivyo tukaambatana nao hadi nyumbani.

Jamaa mmja ambae hakufahamika akikagua mlango wa chumbani jinsi ulivyovunjwa na kuchukua vitu.
“Tulikuta wamevunja mlango na kuzama ndani ambapo chumbani kwangu walichukua tivii flat screen, viatu na nguo zangu, maana kumbe wakati wanaenda chumbani kwangu walijua ni chumba cha Ali.
“Bahati nzuri majambazi walipofika walimwambia yule ndugu yetu aliyekuwa pamoja na mlinzi awaelekeze chumba cha Ali ambapo aliwapotosha kwa kuwaelekeza kwangu.
“Baada ya kuvunja mlango hawakumuona hivyo wakamuuliza akawaambia hajui labda katoka yeye akiwa amelala ndiyo wakaishia kuchukua vitu hivyo vya ndani.
“Wakati wanafanya hayo yote yeye (Ali Kiba) alikuwa akiwasikia tu chumbani kwake maana hadi wanatoka alikuwa akiwafuatilia kwa makini na hata maneno waliyokuwa wakizungumza yalikuwa yakutishia sana amani yake.
“Nashukuru kaka yangu hajaguswa, ila wameiba vitu kibao maana ukiachilia mbali tivii yangu na nguo wamechukua tivii ya sebuleni na kila kitu kilichobebeka,” alisema Abdul Kiba.
Hadi storyi hili inakwenda mitamboni, jeshi la polisi lilikuwa likiendelea na uchunguzi wa kuwasaka watuhumiwa.

Ni vyema mastaa mbalimbali ambao wanaonesha mali zao kama Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wakaimairisha ulinzi nyumbani kwao ili kujilinda zaidi. -Mhariri
photo by:global publishers
On 07:15 by barbrawilliam in ,    No comments

Mashabiki wa Wema Sepetu na Diamond Platnumz..Matusi Hayamjengi Mtu, Yanambomoa!



     
    Kutangaza hapa piga :0718 406 300
    Kwa mashabiki wa Wema Sepetu na Diamond Platnumz. Hawa wawili ni wasanii wetu wanaokubalika nchini, kila mmoja kwa namna yake na kila mmoja ana mashabiki wake. Waliwahi kuwa wapenzi lkn mambo hayakwenda kama mashabiki na wao walivyotaka wakaamua kwa amani kuachana. Lakini bado wanaheshimiana na hata familia zao zinaheshimiana. Na Wema Sepetu bado anamsapoti Diamond ni msanii wake wa kwanza nchini anayependa kazi zake.

    Mpaka hapo, ukishaelewa hayo huwezi kupata ujasiri wa kuwatukana kivyovyote. Hupendi hawako pamoja? Basi support yule unayempenda au kama unawapenda wote wawili endelea kuwasapoti sio kosa lako hawako pamoja! Ni kwa faida yao nzuri tu yenye nia njema. Heshimu mawazo yao...... Sijui khs nia ya team diamond...ila naomba nieleweke kwa wanaompenda Wema... ana projects nyingi zinakuja pia ana issue kubwa nchini ambayo itahusisha watu maalumu ngazi za juu serikalini vile vile si mnaona pia kuna suala la yeye kupigiwa kura?
    Ni kwamba Wema anapendwa na watu wengi, lakini kitendo cha watu wanaotumia jina lake kutukana kitaleta makundi na watu kwa kukomoa watasapoti watu wengine au akiwa na issue hawatamsapoti ambapo si vibaya lkn sababu kubwa ni kwamba watu wanatukana sana.

    Kuna wengine wanatumia kivuli cha Wema lkn ukweli hawampendi na kuna wanaotukana watu sana mpaka watu hudhan Wema anawatuma au team Wema wahuni lkn si kweli, Wema ana watu wengi wanaombeba wenye heshima zao....pia yeye Wema hatukani au kujibizana na watu kuweni kama yeye, msimchafulie mwenzenu.

    Kwa namna hii watu wanaogopa kusema wanampenda Wema hadharani kwa kuhofia kutukanwa hii inampunguzia Wema marafiki. Ukweli ndo huo, sasa kama kweli unampenda Wema onyesha mapenzi yako kumsapoti na sio mwezi mzima unatukana halafu siku moja tu ndo unamsapoti wewe utakuwa sio mpenzi wa Wema.

    Ujumbe wa leo: Matusi Hayamjengi Mtu, Yanambomoa!!!

    By barbra william
    05.05.2015 -  
    facebook:barbrawilliam
    instargram:barbrawilliam 
    On 07:04 by barbrawilliam in ,    No comments


    ROSE NDAUKA NA SHETTA
    Wimbo wa Ruby Na Yule unaweka wazi Vitu ambavyo Vitakufanya uamini kuwa Mama Kaylah Mke wa Shetta Hajarudi nyumbani baada ya Kumwacha Shetta kwa Kile alichokidai kuwa Shetta Amechepuka na Mwanadada wa Bongo Movie Rose Ndauka.
    Kwenye mahojiano ya Juzi Tarehe 29 aliyofanya na Kipindi cha DUNDO cha MJ FM ambapo Shetta alikuwa anaizungumzia Ngoma ya mtu mwingine Ambayo anaikubali Kuliko ambapo aliuchagua wimbo wa Ruby Uitwao NA YULE kama Hit On Chart yake na Hapo ndipo akabanwa na DjHaazu Akazungumza KUPITIA DUNDO HIT ON CHART.
    Kama unaifahamu vizuri ngoma ya Ruby Na Yule Hutapingana na mimi kuwa ni wimbo ambao unaweza Kuudedicate kwa Mpenzi wako Mpyaaaaaaaaa….. Sasa Shetta na Mkewe wamepeana Likizo Kimpango Flani sasa unajiuliza Mpenzi Mpya kwake ni naniiiiiii?
    KILICHOTOKEA HEWANI KISIKILIZE HAPA CHINI NA UJIULIZE JE ANAMMAANISHA ROSE NDAUKA ANGELETWA MAPEMA KWAKE??
    facebook:barbrawilliam
    Instagram: barbrawilliam