Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Make up. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Make up. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 18 Septemba 2015

On 02:40 by barbrawilliam in , , , ,    No comments

lupita6
Hii ni cover ya pili ya Lupita kutoka Vogue ya kwanza ilikuwa mwaka jana July.
 
lupitaonvoguesepember2015 (1)
Yani lipstick hii imemfanya aonekane kapendeza mnooo hapa ,the dress is from GYVENCHY
Ukitaka soma zaidi ingi humu 
lupitaonvoguesepember2015 (1)p
picha iliyonivutia zaidi kwani gauni ni zuri sana na inavutia sana
 
lupitaonvoguesepember2015 (2)
ukiwa kama mwana mitindo unapaswa uwe na mapozi na
muonekano wa kipekee kama mmuonavyo lLupita hapi pichani
  lupitaonvoguesepember2015 (5)
Kuna sehem kwenye interview anasema she does Yoga so hili pozi laeleweka linatoka wapi
lupitaonvoguesepember2015 (3)
1970’S vibes
lupitaonvoguesepember2015 (11)
akitokea machoni mwa watu hakuna anayechoka kumuangalia
 

Alhamisi, 2 Julai 2015

On 04:23 by barbrawilliam in , ,    No comments
How to Get Rid of Pimple Scars Naturally
Asilimia kubwa ya watu wamekuwa na tatizo la kuwa na makovu yanayosababishwa na chunusi kwa kipindi kirefu bila kupata ufumbuzi,  na hii husababishwa  sana na mabadiliko ya miili kipindi cha ujana , au kwa watu wenye nyuso zenye mafuta na baadhi ya watu wamepata matatizo haya  baada ya kutumia baadhi ya vipodozi visivyoendana na ngozi zao. Tatizo hili limekuwa kubwa kwa baadhi ya watu na kuna wakati mtu ana kosa hata raha na kuwa huru  kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na mtu kwa kuogopa muonekano wa madoadoa ya ngozi ya uso wake. Leo  tutaenda kuangalia  moja ya tiba ya kuondoa madoa madoa ya chunusi inayoweza kutengenezwa na mtu yoyote nyumbani bila kutumia gharama kubwa.

Mahitaji
Unga wa Riwa
Maji ya Rose (Rose water)
Maji safi ya kawaida
Limao
Mafuta ya Olive (Olive oil)

Hatua ya Kwanza
Chukua unga wa Riwa na Maji Rose uyachanganye  pamoja na ukoroge hadi mchanganyiko wako uwe mzito.

Hatua ya Pili
Upake mchanganyiko wako katika sehemu yenye makovu na uache hadi ukauke. Unaweza kukaa na huu mchanganyiko huu kwa muda mrefu  ila inategemea na nafasi yako pia, mchanganyiko huu unasaidia kunyonya mafuta na kuacha ngozi kavu.

Hatua ya Tatu    
Nawa  vizuri na maji ya uvuguvugu.

Hatua ya Nne
Paka Juice ya Limao kwenye sehemu yenye makovu.  Juisi ya limao inatumika kama brichi ya asili ambayo husaidia kufifisha madoadoa  na kuondoa makovu kwenye ngozi .

Hatua ya Tano
Paka mafuta ya Olive  kwenye makovu, hii husaidia kulainisha ngozi na kufanya makovu yasionekane kirahisi.


Mambo ya kuzingatia
Wakati unaanza kufanya tiba hii jaribu kuacha kutumia aina ya vipodozi vya kemikali ulivyokuwa unatumia na utumiea hii tiba ya asili isiyo na madhara. Jaribu kufanya zoezi hili walau mara mbili kwa wiki  ndani ya mwezi mmoja utaona matunda yake.

Jumatano, 1 Julai 2015

On 11:52 by barbrawilliam in    No comments

On 11:27 by barbrawilliam in , ,    No comments
Rangi ya mdomo ni moja ya vipodozi vinavyoongeza urembo kwa mwanamke.Kuna rangi mbalimbali za mdomo kulingana na anachopenda kupaka mrembo husika.Kwa mujibu wa wataalamu wa masuara ya urembo unaweza kupaka rangi ya mdomo kulingana na umri,tukio na nguo unazovaa au ulizo vaa siku hiyo
Katika safu hii ya urembo leo nitakujjuza namna ya kuchagua rangi ya mdomo kulingana na umri wako.

           *Wasichana wanashauriwa kupaka rangi za kawaida











*wanawake wanafanya kazi wanashauriwa kutokupaka rangi zinazo ng"ara au zilizokolea wakati wanakwenda kazini.*

    *Wanawake vijana wenye ngozi angavu na umri18na25wanashauriwa kupaka rangi ya pinki.
    *Wanawake wenye ngozi nyeusi kati  ya 18na25wanaweza kupaka rangi za machungwa
     *Wanawake wenye umri25na40 wanashauriwa kupaka rangi zilizopoa.                          .
















Kwa kufanya hivyo,siku zote utajikuta ukiwa na mvuto kwa rangi ya mdomo hata kama una umri mkubwa                                  


Ijumaa, 26 Juni 2015

On 08:08 by barbrawilliam in , ,    No comments
UREMBO ni jambo muhimu kwa mwanamke kwa kujiweka nadhifu wakati wote ikiwa ni pamoja na kujipamba na kujifanyia usafi wa mwili. Watu wengi wamekuwa na uelewa mdogo juu ya masuala ya urembo kwa kudhani kuwa urembo ni kujipaka poda tu usoni na wanja kwenye nyusi huku wakisahau kuwa urembo ni pamoja na kuufanya usafi mwili kwa ujumla
Kwani huwezi kupaka poda kama sura yako si safi.Leo katika safu hii utaona jinsi gani unaweza kubandika kucha za bandi kama una kucha fupi. Kabla ya kubandika kucho hizi hakikisha kucha zako za zsili zinakuwa safi kwa kuziosha na kuzitoa uchafu uliopo ndani ya kucha ili ziweze kuwa safi na kuweza kubandika kucha.
Baada ya kucha hizo kuwa safi unaweza kubandika hizo kucha za bandia bilakusahau kuhakikisha zote zinakuwa katika usawa mmoja tayari kwa ajiri ya kupaka rangi uipendayo. Lakini kumbuka wataaramu wanashauri kucha za bandia zisikae kwa muda mrefu bila kutolewa kwani zinaweza kusababisha kucha halisi kuoza, hivyo wanashauri zitolewe baada ya wiki mbili na si zaidi.

Lakini pia wanashauri kutumia dawa maalumu ya kutolea na si kutoa kienyeji kwani zinaweza kukusababishia maumivu pamoja na kuzifanya kucha halisi kuwa na muonekano mbaya wa mabonde mabonde