Jumanne, 21 Machi 2023
On 06:29 by barbrawilliam in Habari No comments
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema kuwa Bandari Kavu ya Kwala
inatarajiwa kuanza kufanya kazi muda wowote kuanzia sasa na itatoa huduma zote za
kiforodha kama zinavyotolewa katika Bandari zingine.
Akizungumza hivi karibuni kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa,
Meneja Miliki wa Mamlaka hiyo, Alexander Ndibalema ameeleza kuwa, kukamilika kwa
bandari hiyo ni matokeo chanya ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita ambayo
imewezesha takriban Shilingi bilioni 83.247 kutumika katika kuendeleza bandari, ujenzi wa
barabara ya zege yenye urefu wa kilometa 15.5 kutoka barabara kuu ya Morogoro eneo la
Vigwaza kuelekea bandarini na kusogeza miundombinu ya reli mchepuko yenye urefu wa
kilometa 1.3.
"Bandari Kavu ya Kwala ipo tayari kufanya kazi kwa sababu miundombinu yote ya msingi
imekamilika na leseni zingine kutoka mamlaka zingine za Serikali zimeshakamilika ambapo
kinachosubiriwa kwa sasa ni kupata leseni kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)",
alisema Ndibalema.
Ndibalema ameongeza kuwa, lengo kuu la kuanzisha bandari hiyo ni kuongeza ufanisi na
kiasi cha shehena inayohudumiwa katika bandari ya Dar es Salaam, kupunguza msongamano
katika bandari ya Dar es Salaam, kuongeza mapato ya Serikali kupitia huduma zitolewazo
katika Bandari. Hivyo wateja kutoka sehemu mbalimbali wataweza kuchukulia mizigo yao
ndani ya bandari hiyo ambayo ina uwezo wa kuhudumia wastani wa makasha 823 kwa siku
sawa na makasha 300,395 kwa mwaka sawa na asilimia 30 ya makasha yote
yanayohudumiwa katika Bandari ya Dar es Salaam kwa sasa.
Vile vile amefafanua kuwa, bandari hiyo ni ya kimkakati kwa sababu eneo la Kwala lina
miradi mingi ya kimkakati ambayo imeanza kutekelezwa ikiwemo ujenzi wa viwanda
mbalimbali na ujenzi wa Mji mpya wa Kwala, hivyo ni matarajio kuwa mizigo ya Wawekezaji
kutoka nchi mbalimbali inayokwenda kwenye viwanda itachukuliwa hapo.
Ameeleza kuwa, bandari hiyo inatarajiwa kuchangia kwa kiwango kikubwa katika Pato la
Taifa ambapo sehemu kubwa ya mizigo itakayohudumiwa katika bandari hiyo ni ile
inayokwenda nchi jirani.
Bandari hiyo imejengwa kwa awamu mbili zilizojumuisha usafishaji wa eneo lenye ukubwa
wa Hekta 60 na ujenzi wa ukuta uliogharimu Shilingi 9,465,643,798.00, ujenzi wa Yadi hekta
5 kiwango cha zege uliogharimu Shilingi 36,670,971,842.00, ujenzi wa Reli Mchepuko yenye
urefu wa KM 1.3 uliogharimu Shilingi 677,328,320.00 na ujenzi wa barabara yenye urefu wa
KM 15.5 kwa kiwango cha zege uliogharimu Shilingi 36,432,867,115.70 ambayo imekamilika
kwa asilimia 100.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Search
Popular Posts
-
Akiwa na umri wa miaka 89 aliishi katika kipindi kigumu katika miaka ya 1990 kutokana na talaka za watoto wake 3 na ukimya usiokifani...
-
ALLY REHMTULAH KUJA NA UFAHARI WETU FESTIVAL Mbunifu wa mavazi nchini Tanzania Allyrehmtullah ameandaa tamasha linalokwenda kwa jina ...
-
Msanii wa filamu nchini ambaye pia ni Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu, kufungua duka kubwa la urembo nchini Afrika Kusini. Kwa mujibu wa c...
-
Rangi ya mdomo ni moja ya vipodozi vinavyoongeza urembo kwa mwanamke.Kuna rangi mbalimbali za mdomo kulingana na anachopenda kupaka mrembo h...
-
MISS KINONDONI 2019 PRESS BONANZA Leo miss kinondoni wamefanya special bonanza kwa lengo la kuchangia kituo ch...
-
Tamasha la kutuza watu weusi wanaon"ara kwenye fani tofauti zinazoandaliwa na televison(BET),zilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita na...
-
Huyu ni binti mwenye umri wa miaka19 mzaliwa wa mkoa wa Morogoro amemaliza elimu yake ya msingi na sekondani mkoani morogoro. Fani ya urem...
-
barbra william Hatari sana! Mkali wa Ngoma ya Chekecha Cheketua, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ amenusurika kifo baada ya kuvamiwa nyu...
0 maoni:
Chapisha Maoni