Jumapili, 28 Juni 2015

On 00:41 by barbrawilliam in , ,    No comments

Magadi Soda:

Magadi soda ni mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Changanya kiasi kidogo cha magadi soda na maji ya kutosha kuunda kidonge kidogo na kisha weka au kandika kidonge icho sehemu ilio athirika na chunusi. Kwa muda wa dakika 15-20 au mpaka ikauke, na kisha suuza kwa maji yasiwe ya moto. Unaweza kurudia rudia mara kadhaa kwa siku mpaka utakapo ona athari ya chunusi imepotea.

Matango:

Unaweza kutumia Tango kwa kuondoa cna hata kuondoa mabaka mabaka katika ngozi na kuifanya ngozi yako kuonekana yenye afya na yenye kuvutia.
mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Kata tango na kasha liponde ponde (unaweza kutumia blenda) kisha paka au kandika usoni. Wacha ikae kwa muda wa dakika 15-20  kisha suuza kwa maji baridi. Unaweza kurudia kwa siku mara mbili mpaka mara tatu kwa siku.

Image result for kitunguu saumu  Kitunguu Thaumu:

Unaweza kutumia kitunguu thaumu. Kuondoa chunusi. Matumizi ya Kitunguu thaumu, uleta matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na hata kuuwa bacteria sababu ina kemikali (antiseptiki) inayozuia kukua kwa bakteria kwenye jeraha au ngozi iliyo athirika kwa chunusi au hata kwenye kidonda. Na pia ina viwango vya juu wa salfa (ni zuri kwa ajili kukausha mafuta kwenye ngozi ya mwili). Twanga kitungu thaumu, au unaweza kukata nusu na kubandika sehemu iliyo na chunusi shikilia kwa dakika 5-10, na kisha safisha na maji baridi. Waweza kufanya ivyo asubuhi na jioni.

Mnana (Peppermint):

Unaweza kutumia majani ya Mnanaa kuondoa chunusi usoni.
Majani ya manna utumika hata kwa wale wenye matatizo ya Mba kwenye kichwa. Twanga majani machache au saga kisha weka sehemu iliyo athirika. Wacha mpaka pakauke na kisha safisha kwa maji baridi. Unaweza kufanya hivyo mara kadhaa kwa siku.

Matumizi ya Limao:

Kata limao na kisha kwa kutumia kihenye pamba kiloweke kwa maji ya limao, sugua sehemu yenye chunusi, kisha wacha pakauke, unaweza kurudia rudi kila baada ya masaa kadhaa. Usitumie maji ya limao ya kwenye chupa, kwa sababu yameweka vihifadhi kemikali zingine kiasi cha kuondoa ubora wa kemikali halisi za kwenye limao. Tumia limao alisi.

Kutumia Asali:

Matumizi ya asali ni ya asili na ufanya ngozi, iwe na afya na nyororo. Kwa sababu kwenye asali kuna virutubisho vingi vyenye kazi ya kuua vimelea (bacteria) na kuzuia uchafu na kusinyaa kwa ngozi.
Weka asali kidogo sehemu ilio athirika na iwache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Vilevile unaweza kupaka uso mzima au hata mwili mzima ukitaka. Sababu asali inarutubisha ngozi ya mwili na kuifanya iwe na afya na mwonekano mzuri. Ukisha ridhika na muda wa asali kwenye ngozi yako unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya vuguvugu.

Kutumia Papai:

Unaweza kushangaa, lakini matumizi ya paameonyesha matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na kusafisha sehemu zingine za mwili.
Ponda ponda kiasi kidogo cha papai na kisha iwache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Ukisha ridhika na muda unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya kawaida. Unaweza kurudia mara kadhaa kila siku kama unataka.

Dawa Ya Meno:

Unaweza kushaini ushangazwi na matokeo mazuri ya meno yako kusafishika kwa dawa ya meno.
Image result for dawa ya meno
Kemikali zinazotumika kuuwa Bakteria wa kwenye meno, pia zina uwezo wa kupambana na bakteria wengine. Tumia dawa ya meno isiyo na gel (non-gel) paka kwenye chunusi. Ni vizuri ukatumia usiku wakati wa kwenda kulala, ila si vibaya ukipaka hata muda wa asubuhi au mchana mradi tu uwe na muda wa kutosha wa dawa kukauka ili iweze kufanyakazi vizuri.

Namna nyingine ni kuchanganya dawa ya meno na unga wa mahindi au nganoiuliosagwa na kuwa laini sana. Unaweza kupaka na kuiwacha ikauke kwa dakika tano mpaka 10.

Safisha kwa sabuni. Mchanganyiko huu unasaidia kukausha chunusi.

Matumizi ya Poda:

Image result for Baby powderUnaweza kutumia baby powder kwa kupaka nyakati za usiku wakati wa kwenda kulala na na kuiwacha mpaka asubuhi.

Matumizi ya Mvuke:

Unaweza kutumia mvuke (Steam/vapour) kuondoa mafuta yaliozidi kwenye ngozi ya uso wako. Kwa kujifukisha. Kwa wale ambao hawana mashine wanaweza kujaza sufuria au bakuli kwa maji ya moto na kujifunika kwa taulo uku ukielekeza uso wao kwenye sufuria au bakuli lenye maji yanayotoa mvuke k wa dakika 5-10. Unaweza kufanya hivi pamoja na njia mojawapo nilizo zitaja hapo juu.

Tahadhari:

Njia hizi za Asili, uchukuwa muda kidogo mpaka kuona matoke ya kuridhisha.
Njia zote hizi kama hazijaleta matokeo mazuri, tafadhali muone daktari wa ngozi au nenda hospitali ilio karibu kwa uchunguzi zaidi wa ngozi yako.
On 00:27 by barbrawilliam in , ,    No comments

Faiza Ally ameingia kwenye vita kubwa ya maneno na msanii Peter Msechu baada ya msanii huyo wa bongo fleva  ujumbe mzito.Leo asubuhi Peter Msechu ameitwa kubwa jinga na mwanamama huyo na kuambiwa bila mashindano ya bongo star search sijui angekuwa wapi.

Peter Msechu alitoa ya moyoni kulaani kivazi hicho kwa siku muhimu kama ile ambapo hadi viongozi wa serikali huudhulia na wasanii kupata nafasi ya kupewa kipaumbele nchi nzima na kutazamwa.

Huyu ni mke wa mheshimiwa mmoja hiviiiiiiiii, la haulaa! hapa ndipo tumefikia

Mama huyo wa mtoto mmoja Sasha amedai watu wengi wamemfahamu kupitia kivazi hicho wasimuhukumu.Amefanya mengi na makubwa kwenye jamii,anasomesha watoto yatima nakujishuhulisha na kampeni za mauaji ya albino na magojwa ya kansa.

Na katika uhalisia kivazi hicho kilishuka bahati mbaya na kushindwa kupandisha.Watu maarufu walio laani tendo hilo kwa kumsapoti Peter Msechu ni Diamond Platnum,Kajala,Shilole,Jokate,Salama Jabir,Joe Makini,Jokate na Madam Lita kwa kulike ujumbe huo
.
On 00:22 by barbrawilliam in , ,    No comments


 


Image result for NGUO ZA USIKU

Ijumaa, 26 Juni 2015

On 08:08 by barbrawilliam in , ,    No comments
UREMBO ni jambo muhimu kwa mwanamke kwa kujiweka nadhifu wakati wote ikiwa ni pamoja na kujipamba na kujifanyia usafi wa mwili. Watu wengi wamekuwa na uelewa mdogo juu ya masuala ya urembo kwa kudhani kuwa urembo ni kujipaka poda tu usoni na wanja kwenye nyusi huku wakisahau kuwa urembo ni pamoja na kuufanya usafi mwili kwa ujumla
Kwani huwezi kupaka poda kama sura yako si safi.Leo katika safu hii utaona jinsi gani unaweza kubandika kucha za bandi kama una kucha fupi. Kabla ya kubandika kucho hizi hakikisha kucha zako za zsili zinakuwa safi kwa kuziosha na kuzitoa uchafu uliopo ndani ya kucha ili ziweze kuwa safi na kuweza kubandika kucha.
Baada ya kucha hizo kuwa safi unaweza kubandika hizo kucha za bandia bilakusahau kuhakikisha zote zinakuwa katika usawa mmoja tayari kwa ajiri ya kupaka rangi uipendayo. Lakini kumbuka wataaramu wanashauri kucha za bandia zisikae kwa muda mrefu bila kutolewa kwani zinaweza kusababisha kucha halisi kuoza, hivyo wanashauri zitolewe baada ya wiki mbili na si zaidi.

Lakini pia wanashauri kutumia dawa maalumu ya kutolea na si kutoa kienyeji kwani zinaweza kukusababishia maumivu pamoja na kuzifanya kucha halisi kuwa na muonekano mbaya wa mabonde mabonde
On 04:32 by barbrawilliam in ,    No comments
Hili ni jambo ambalo wamekuwa wakilipenda watu wengi lakini hujikuta kwenye wakati mgumu hasa linapokuja suala la uchaguzi wa mavazi hayo. 

Umewahi kutamani kuwa na mwonekano wa kimavazi unaoendana na mwenza wako na hujui ufanye nini?

Hili ni jambo ambalo wamekuwa wakilipenda watu wengi lakini hujikuta kwenye wakati mgumu hasa linapokuja suala la uchaguzi wa mavazi hayo. 

Ugumu huu utokea mara nyingi katika kupata nguo ambayo inaweza kuvaliwa na mwanamke na mwanaume bila kuleta muonekano wa ajabu.

Zamani hili lilikuwa likiwezekana kwa urahisi kwa kutumia vitenge lakini siku hizi jambo hili limekuwa likiwezekana kutokana na kuwapo nakshi za kila aina kwenye mitindo. 

Wabunifu wa masuala ya urembo wanasema unaweza kutumia aina yoyote ya mavazi na kushona kwa mtindo muutakao.

Sambamba hilo pia mnaweza kutumia rangi za aina moja wakati mnachagua mavazi yenu. 

Kuvaa nguo zinazofanana na mpenzi wako haijalishi ni sehemu muhimu kama katika dhifa mbalimbali bali pia mnaweza kuwa na kawaida ya kuvaa mavazi hayo katika mitoko yenu ya kawaida kama ofisini, mnapokuwa katika matembezi katika fukwe za bahari pia hata mnapoenda kufanya ununuzi wa bidhaa zenu za nyumbani.

Mnaweza kuvaa suruali za jeans na tisheti au mashati yanayofanana lakini pia mnaweza kushona nguo ambazo zitakuwa na nakshi ya kitenge au khanga na wote mkaonekana mmeng’ara. 

Bazee pia linaweza kushonwa nguo za jinsi zote na kuleta mwonekano mzuri kwa wavaaji mnapoongozana pamoja.

Mnaweza pia kuchagua nguo za rangi zinazofanana hata kama zitakuwa katika mitindo tofauti lakini bado mtaonekana mmependeza. Hapa mwanamke anaweza kuvalia nguo yake yoyote na ili kwenda sambamba na mwenzi wake basi ataangalia moja ya rangi zilizopo katika gauni hilo na yeye akavaa shati na wote wakaonekana wanapendeza.

Wakati mwingine si lazima kuvaa nguo zinazofanana bali pia mwanaume anaweza kutumia tai yenye rangi zinazofananana nguo ya mwenzi wake. Hapa anaweza kuvaa tai ndevu au fupi ili mradi iwe na rangi ambazo zipo katika nguo ya mwezi wake.

Kwa kufanya hivyo muda wote wewe na mpenzi wako mtaonekana mnapendeza na kuvutia machoni kwa watu.

Jumanne, 9 Juni 2015

On 05:12 by barbrawilliam in ,    No comments

mzee kanka amefariki

Taarifa zilizonifikia hivi punde kuwa Msanii wa Maigizo aliwahi kucheza michezo ya Tv uliyojulikana kama Jumba la Dhahabu Mzee Kanka amefariki Dunia chanzo cha kifo chake bado tunazifuatilia endelea kuwa nasi tutakujulisha.