Alhamisi, 2 Julai 2015
On 01:58 by barbrawilliam in Afya No comments
Maambukizi ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa na uwepo wa fangasi wanaojulikana kitaalamu kama Candida albicans. Maambukizi haya pia hujulikana kama yeast infection au thrush. Fangasi hupatikana kama vimelea vya kawaida katika mdomo, mpira wa kupitisha chakula sehemu inayojulikana kama pharynx, katika kibofu cha mkojo, uume na hata kwenye uke.
Mfumo mzuri wa kinga wa mwili pamoja na aina fulani za bakteria wanaoishi pamoja na fangasi husaidia sana katika kuthibiti maambukizi yanayoyosababishwa na aina hi ya fangasi.
Kwa kawaida, Candida albicans huishi kwenye uke na sehemu nyingine kama zilivyoelezewa hapo juu bila kusababisha madhara yoyote yale isipokuwa pale mazingira ya eneo husika yanapobadilika kama vile mabadiliko katika hali ya PH ya eneo husika (ifahamike ya kwamba pH ya kawaida ndani ya uke ni 4.0 – 4.5) au uwiano wake na vimelea (microorganisms) lakini pia uharibiwa kutokana na sababu mbalimbali kama vile matumizi ya madawa aina ya antibiotics na kupungua kwa kinga mwilini kutokana na magonjwa mbalimbali n.k.
Maambukizi haya ya fangasi yanaweza kugawanywa katika sehemu kuu mbili;
- Maambukizi yasiyo makali yaani ‘uncomplicated thrush’ kwa kiingereza:
- Maambukizi makali yaani ‘complicated thrush’ kwa kiingereza:
Kwa kawaida Watu walio katika hatari ya kupata maambukizi ya fangasi hawa ni wale wenye;
- Kutumia sana dawa aina ya detergents kwenye sehemu za siri au douches (vifaa vinavyotumiwa kusafishia uke kwa kutumia maji yaliyochanganywa na jiki au antiseptic yoyote ile) kwa sababu hali hiyo husababisha kuharibika kwa uwiano wa fangasi na aina nyingine ya vinyemelezi kama bakteria aina ya lactobacilli
- Kutumia sana madawa aina ya antibiotics, steroids ambayo yana tabia ya kushusha kinga ya mwili
- Ugonjwa wa ukimwi (HIV/AIDS) n.k
ANGALIZO Wanawake wenye umri wa miaka kati ya ishirini na thelathini wapo kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi haya wakati wale ambao wameshaacha kupata hedhi au wale ambao hawajaanza kupata hedhi kabisa hawako kwenye hatari kubwa.
Dalili na viashiria kwa wanawake;
- Kuwashwa sehemu za siri (kwenye tupu ya mwanamke)
- Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri (burning sensation)
- Kufanya kama vidonda katika sehemu za siri (soreness)
- Maumivu wakati wa kujamiana (superficial dyspareunia)
- Maumivu au usumbufu wakati wa kujisaidia haja ndogo (wakati mtu anakojoa)
- Kuvimba na kuwa rangi nyekundu kwa mdomo wa nje wa tupu ya mwanamke (labia minora)
- Kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au nyeupe kijivu, unaoweza kuwa mwepesi, majimaji au mzito na ambao umefanana na jibini (cottage cheese like discharge) wenye muonekano unaojulikana pia kama curd-like appearance. Kwa kawaida, uchafu huu haumbatani na harufu yoyote isipokuwa panapokuwa na tatizo la ziada kama ugonjwa wa zinaa aina ya Bacteria vaginosis. Uchafu huu unaotoka hapa unaweza kuenea kwenye maeneo mengine yaliyokaribu na tupu ya mwanamke kama kwenye mitoki (groin area) au perineum na kusababisha kuharibika kwa ngozi katika sehemu hizo.
Dalili na viashiria hivi huwa mbaya zaidi wakati mwanamke anapokaribia kupata hedhi.
Dalili na viashiria kwa wanaume ni;
- Kuwashwa sehemu za siri
- Kuvimba na kuwa rangi nyekundu kwenye ncha ya uume
- Kuwepo kwa uchafu wa rangi nyeupe (kama nilivyoeleza hapo juu) kwenye sehemu ya juu ya uume.
- Kuwa na vidonda vidogo kwenye uume (sore on the glans)
Hata hivyo, mara nyingi wanaume hawaoneshi dalili zozote zile, ni vizuri kwa mwanamke kumueleza mwenza wake pale anapopata maambukizi haya ili naye pia apate kutibiwa.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Search
Popular Posts
-
Msanii wa filamu nchini ambaye pia ni Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu, kufungua duka kubwa la urembo nchini Afrika Kusini. Kwa mujibu wa c...
-
WENGI ukiwauliza kuwa wanamfahamu vipi Kojate Mwegelo, jibu lao litakuwa ni Mshindi wa pili wa Miss Tanzania mwaka 2006. Wengine ...
-
Hii ni baada ya taarifa siku ta jana kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na watu wengi kushangaa kwanini Miss Tanzania 2020-2021 Rose...
-
ALLY REHMTULAH KUJA NA UFAHARI WETU FESTIVAL Mbunifu wa mavazi nchini Tanzania Allyrehmtullah ameandaa tamasha linalokwenda kwa jina ...
-
KAA UKITAMBUA KUWA MKE NI MATUNZO, YAANI SAWA NA MGOMBA KUPALILIWA KILA WAKATI!!! Assalaam alaikum/Bwana Yesu asifiwe! Bila shaka mna afya ...
-
Msanii wa Movie hapa nchini Elizabeth Michel a.k.a Lulu amefunguka haya mambo matano kuhusu chama anachokipenda na ni nani atampigia kura...
-
Akiwa na umri wa miaka 89 aliishi katika kipindi kigumu katika miaka ya 1990 kutokana na talaka za watoto wake 3 na ukimya usiokifani...
-
MISS KINONDONI 2019 PRESS BONANZA Leo miss kinondoni wamefanya special bonanza kwa lengo la kuchangia kituo ch...
-
Tarehe kama ya leo julai 18 mwaka 1918 alizaliwa,Mzee Nelson Mandela Raisi wa kwanza wa Africa kusini alichaguliwa kidemokrasia na ni mshind...
-
JINSI YA KUMTAMBUA MWANAMKE ANAYEKARIBIA KUKUACHA! Kuna tofauti kubwa ya kimaamuzi kati ya mwanaume na mwanamke kwenye suala la k...
Recent Posts
Categories
Sample Text
Blog Archive
-
▼
2015
(56)
-
▼
Julai
(11)
- MAYUNGA NALIMI AIRTEL TRACE MUSIC STAR
- JINSI YA KUJIWEKA WA THAMANI KWA MPENZI WAKO
- Miti shamba inayofanya matiti kuwa makubwa na yal...
- JE? UNAMFAHAMU LINAH SANGA NJE NA MUZIC ANAJISHUGH...
- BREAK NEWS;UJIO WA LOWASA CHADEMA WAWAGAWA MBOWE N...
- STAA NA MTOKO TOFAUTI NDANI YA BET
- MNYAMA MWENYE SAUTI KUBWA DUNIANI
- FAIDA YA LIMAO KWENYE NGOZI
- FANGASI SEHEMU ZA SIRI
- PENDEZA KWA KUPAKA MAKE UP KUTOKANA NA KIREMBA ULI...
- CHAGUA RANGI YA MDOMO KUTOKANA NA RANGI YAKO
-
▼
Julai
(11)
0 maoni:
Chapisha Maoni