Alhamisi, 16 Julai 2015

On 07:37 by barbrawilliam in , ,    No comments
Msanii Linah Sanga alimaarufu kama Ndege mnana amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye nje ya kazi yake ya sanaa ni msusi mzuri

wa nywele na alikuwa akifanya kazi hiyo toka akiwa shuleni na anaipenda hivyo anadai mpaka sasa bado anaipenda na anazidi kujifunza mambo mbali mbali yanayohusu urembo na ususi sababu ni kitu anachokipenda.


Linah alisema kuwa kipindi alipokuwa shule alikuwa maarufu sana kwa ususi kwa kuwasuka watu nywele ingawa alikuwa analipwa ujira mdogo wa shilingi mia tano lakini alikuwa anapenda kile alichokuwa akikifanya na alikuwa anafurahi kuona anawasuka wanafurahi kusukwa vizuri na yeye
.


Unajua mimi napenda sana ususi toka nikiwa shule nilikuwa nawasuka wenzangu ingawa walikuwa wakinilipa pesa ndogo Shilingi mia tano lakini nilikuwa napenda kuwasuka na walikuwa wanapendeza hivyo hali hiyo iliendelea hata nilipokuwa nyumbani kuna watu nilikuwa nawasuka hivyo kusuka ni kipaji changu nje ya muziki nao fanya sasa, najitahidi sana niweze kuwa na Salaoon yangu
.


"Unajua mimi jina langu kwa sasa ni kubwa na thamani yake pia hivyo siwezi kusema nifungue tu kiji-Saloon bali napaswa kufungua Saloon kubwa yenye sifa la jina langu, kiasi kwamba hata mtu akiangalia na kuaambiwa hii Saloon ya Linah aweze kukubali na kuona yes nimefanya jambo, ndiyo maana nasema inabidi nijipange kwanza ili niweze kufanya hilo.


Linah anakiri wazi kuwa ususi ni kipaji chake lakini anasema kutokana na kuwa busy na masuala ya muziki kipaji chake hicho cha ususi kimekaa pembeni japo anaamini kuwa anaweza kukiendeleza na kufanya mwenyewe hiyo kazi na kwenda sawa na mabadiliko ya mitindo ya nywele yaliyopo kwa sasa


" Ingawa kwa sasa kuna style nyingi za ususi hivyo naamini hazinitoi jasho inabidi kujifunza tu na kufanya sana mazoezi ila ninaweza kujifunza na kuvijua vitu vingine vingi zaidi vinavyohusiana na ususi na mambo ya urembo kama nitajifunza na kujiongeza " Aliongeza Linah Sanga

0 maoni:

Chapisha Maoni