Jumatatu, 13 Julai 2015

On 08:38 by barbrawilliam in ,    No comments
Hali ndani ya chadema imezidi kuwa tete mpaka sasa baada ya katibu mkuu wa Chadema Dr.slaa kutishia kurudisha kadi ya Chadema  na kuachana na siasa za chama hicho kama MBOWE ataendelea kumshawishi na kumuomba LOWASA kujiunga na chama hicho ili awe mgombea wao wa uraisi.
Dr.SLAA ameonyesha msimamo huo muda mfupi kabla ya LOWASA hajaongea na waandishi wa habari nyumbani kwake masaki kuhusiana na hatima yake hiyo.Slaa amekihakikishia chambo  chetu kwamaba yeye hamuungi mkono MBOWE kwenye mpango wake huo wa kumtaka LOWASA awe mgombea wa urahisi kupitia chama hicho.
Kijana mmoja wa CHADEMA ambaye yupo karibu na MBOWE amethibitisha kwamba MWENYEKITI wao huyo yupo tayari hata kumfukuza chama SLAA ili LOWASA  awe mgombea wao anasema MBOWE anaamini kwamba LOWASA ataipeleka CHADEMA madarakani
Kwasababu ya mpasuko huo,timu ya mkakati ya LOWASA imeamua kuahirisha  mkutano wao na Waandishi wa Habari uliokuwa ufanyike leo saa tano asubuhi hii kama ambavyo Mbowe ameomba ili kwanza wamalize tofauti zilizojitokeza kati yake na SLAA.Ikumbukwe kwamba  hivi sasas SLAA ana mvutanao mkubwa na viongozi wenzake wa UKAWA ambapo analazimisha yeye awe mgombea.

Tayari  mzee EDWIN MTEI ametumiwa  ndege ili aje Dar haraka kumshawishi SLAA akubali kumpisha LOWASA kugombea urais

0 maoni:

Chapisha Maoni