Jumatatu, 20 Julai 2015

On 10:03 by barbrawilliam   No comments
Mayunga 3Fainali ilikua ni Jumamosi ya April 18 2015 ambapo shindano la Airtel Trace Music Stars lilifanyika Nairobi Kenya likiwa ni shindano la kumtafuta mkali wa kuimba ambapo zilishirikishwa nchi 13 kutoka Afrika na Mtanzania Mayunga Nalimi ndio akashinda.
Kivutio kingine kikubwa kwenye hili shindano lililoandaliwa na kituo kikubwa cha TV chaUfaransaTRACE Urban, kilikua ni Akon, mwimbaji maarufu aliyezaliwa St. Louis, Missouri Marekani miaka 41 iliyopita lakini maisha yake ya utoto yakapitia pia mikononi mwa Senegal.
Mayunga 2Kwenye picha ya kwanza juu ni Akon akiwa Jaji pamoja na  Lynnsha na Devyne Stephens ambao wakati Mayunga anaimba wimbo wa mwisho kabla ya mshindi kutangazwa, walisimama kwa ishara kwamba wamemnyooshea mikono Mtanzania huyu kwa ukali au kipaji kikubwa alichokionyesha kwenye uimbaji.
Mayunga Trace 1
Hii ni wakati Manyunga alipotangazwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars Tanzania
Mayunga 4
Mayunga kwenye fainali Nairobi, hii ilikua ni muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi.
Super star huyu mpya amezaliwa ambapo miongoni mwa vitu atakavyovifanya ni kuungana na Akon kwenye studio yake huko Marekani kwa ajili ya kurekodi single yake ya kwanza (Mayunga)

0 maoni:

Chapisha Maoni