Ijumaa, 22 Mei 2015
On 04:05 by barbrawilliam in Afya No comments

IMEELEZEWA na wachunguzi kwamba sababu ambayo humfanya mwanamme mwenye afya kutoa mbegu zaidi ya milioni 40 wakati wa tendo la ndoa na mbegu moja tu ya kiume na ya kike hutakiwa katika kutunga mimba, ni “kushindana kwa mbegu za kiume”.
Kwa wastani, mwanamme hutoa kiasi cha mbegu bilioni 525 katika maisha yake, na kwa kila mwezi hutoa mbegu hizo zisizopungua bilioni moja.
Kwa upande wa wanawake, wao huwa wamezaliwa na mayai milioni mbili ya uzazi, na wafikiapo wakati wa balehe, idadi kubwa ya mayai hayo hujifunga na kuacha mayai 450 tu ambayo huweza kukomaa na kuwa mayai yenye uwezo wa kutunga mimba.
Kulingana na utafiti mpya, tangu zama za kuwepo kwa jinsia za kiume na kike, jinsia ya kiume imekuwa na ushindani katika kutaka kupeleka mbegu zake za uzazi karibu na yai la kike. Katika ushindani huo msingi wake ni kwamba kufikisha mbegu za kiume karibu na yai la kike kunatoa uwezekano mkubwa zaidi wa kuungana na yai la kike na kutunga mimba. Hivyo jinsia ya kiume huitafuta fursa hiyo kwa kutia maanani kwamba ni “mimi naweza kufanya hivyo na si jirani yangu”.
Mashindano haya ni mabadiliko ya lazima kwa viumbe wa kiume wa aina zote. Iwapo mbegu ya mpinzani wako itafanikiwa kuungana na yai na kutunga mimba, hivyo fursa ya wewe kuendeleza vinasaba vyako kwa viumbe wengine hupotea. Katika vizazi vingi vilivyopita matokeo yamekuwa ni hayohayo: kwamba nguvu za kuzaliana huenda kwa viumbe vya kiume vinavyotoa mbegu nyingi zaidi za uzazi, na hivyo kuweza kuendeleza vinasaba (genes) vyake.
Hivyo, vinasaba vya viumbe wanaotoa mbegu ndogo za uzazi hatimaye hutoweka katika jumuia ya viumbe husika na kubakia tu katika historia ya mabadiliko.
Kama lingekuwa ni suala la kutoa mbegu nyingi ni vizuri zaidi, basi wanyama wa aina zote wangekuwa na korodani kubwa ajabu katika jitihada za kutaka kushinda mashinano ya utoaji mbegu nyingi. Hata hivyo, hilo pekee halitoshi, kwani idadi ya mbegu ni jambo muhimu pamoja na ukaribu wake na yai la kike.
Katika kulifanya yai la kike litunge mimba, si jambo tu la kutegemea manii nyingi unayotoa, bali ukaribu wa manii hayo na yai la kike ni jambo muhimu pia.
Jibu hili limetolewa na Scienceline, mradi wa Mpango wa Habari za Science, Afya na Mazingira wa Chuo Kikuu cha New York.
POSTING BY ;BARBRA WILLIAM
DATE;22/MAY/2015
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Search
Popular Posts
-
ALLY REHMTULAH KUJA NA UFAHARI WETU FESTIVAL Mbunifu wa mavazi nchini Tanzania Allyrehmtullah ameandaa tamasha linalokwenda kwa jina ...
-
Akiwa na umri wa miaka 89 aliishi katika kipindi kigumu katika miaka ya 1990 kutokana na talaka za watoto wake 3 na ukimya usiokifani...
-
Rangi ya mdomo ni moja ya vipodozi vinavyoongeza urembo kwa mwanamke.Kuna rangi mbalimbali za mdomo kulingana na anachopenda kupaka mrembo h...
-
Msanii wa filamu nchini ambaye pia ni Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu, kufungua duka kubwa la urembo nchini Afrika Kusini. Kwa mujibu wa c...
-
JACKSON KABIRIGI'S PROFILE
-
MISS KINONDONI 2019 PRESS BONANZA Leo miss kinondoni wamefanya special bonanza kwa lengo la kuchangia kituo ch...
-
Tanzania ni moja ya nchi zilizoko chini ya jangwa la sahara afrika imekuwa na wimbi la kuongezeka kwa watu wenye ulemavu ngozi ,jamii y...
-
Msanii Linah Sanga alimaarufu kama Ndege mnana amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye nje ya kazi yake ya sanaa ni msusi mzuri wa nywele na al...
Recent Posts
Categories
Sample Text
Blog Archive
-
▼
2015
(56)
-
▼
Mei
(12)
- Kwa nini wanaume hutoa mamilioni ya manii katika k...
- Hisia nane hatari katika mapenzi
- Aina 10 ya Wanawake Wanaopendwa na Wanaume
- Hatua 5 za kuzungumza na mpenzi wako aliyekasirik...
- JINSI YA KUMTAMBUA MWANAMKE ANAYEKARIBIA KUKUACHA...
- MESEJI NZURI ZA MAPENZI KWA UMPENDAYE KWA DHATI ...
- Updated Eyebrow Tutorial
- DIY Turn Your Old Pants Into Cool Bleached, Distre...
- BEYONCE has outdone Kim Kardashian’s and Jennifer ...
- A-Z ALI KIBA ALIVYONUSURIKA KUUAWA!
- Mashabiki wa Wema Sepetu na Diamond Platnumz..Matu...
- SHETTA “NAMUOMBA MUNGU ANGEMLETA ROSE NDAUKA MAPEM...
-
▼
Mei
(12)
0 maoni:
Chapisha Maoni