Jumapili, 28 Juni 2015

WENGI ukiwauliza kuwa wanamfahamu vipi Kojate Mwegelo, jibu lao litakuwa ni Mshindi wa pili wa Miss Tanzania mwaka 2006.
Wengine watakuambia ni Miss Temeke mwaka 2006 na pia Balozi wa bia ya Redds wa mwaka huo huo. Kuna kundi la watu watakujibu kuwa ni mrembo aliyefanikiwa sana katika medani ya urembo.
Majibu yote hayo ni sahihi, hata hivyo kuna mengi ambayo wengi hawayafahamu kuhusu mrembo huyu. Jokate ana vipaji lukuki, vipaji ambavyo anasema ndivyo vinavyomuweka mjini.

Tofauti na urembo, Jokate ana uwezo mkubwa katika uigizaji wa filamu, kipaji chake katika kuigiza kimeonekana katika filamu ya ‘Fake Pastors’ ambayo alicheza kama mtoto wa mzee wa kanisa lakini hakuwa na maadili mazuri. Mbali na kuwa na uwezo mkubwa katika kucheza filamu, Jokate pia ni Mwendesha shughuli mbali mbali, maarufu MC, kazi ambayo kwa mujibu wa mrembo huyu, inamsaidia kuongeza kipato chake.
Kwa kuonyesha kuwa ana vipaji vingi, mrembo huyo alishinda mchujo wa kuwania nafasi ya kuwa mtangazaji wa kituo maarufu cha televisheni cha Channel O cha Afrika Kusini mwaka jana.

Jokate anasema haikuwa kazi rahisi kwake kufanikisha mahojiano mbalimbali katika matamasha nchini humo ambapo alikuwa akihoji watu mbalimbali maarufu wakati wa ‘Red Carpet.’
“Niliweza kuwahoji zaidi ya wasanii 200 na mahojiano yote yalikuwa moja kwa moja , nilianza kwa kuogopa, lakini nilipiga moyo konde na kuendesha mahojiano hayo kwa ustadi mkubwa, najivunia kuwa Mtanzania wa kwanza kutangaza katika kituo hicho.” anasema Jokate
.

“Watanzania wengi wanajua kwa nini Afrika Kusini ipo juu kimuziki na hata katika fani nyingine mbali ya michezo, ni nchi ambayo ina watu maarufu wengi (celebrities), wote hawa kabla ya kuingia katika ukumbi, ilikuwa lazima wapitie kwangu na kuhojiwa, ilikuwa kazi kubwa ambayo imeweza kuniongezea uzoefu mkubwa katika fani ya utangazaji.” anasema.
Anafafanua kuwa kwa sasa bado ni mtangaziji wa kituo hicho, ingawa hurekodi vipindi vingi kabla ya kurejea nyumbani kuendelea na shughuli zake nyingine.
Anasema kuwa utaratibu wa Channel O umemwezesha kuingia katika fani nyingine ya ubunifu wa mavazi ambapo kwa sasa ameibuka na staili mpya ijulikanayo kwa jina la Kidoti
.

Maonesho ya mavazi Jokate ameshiriki maonesho ya mavazi mawili makubwa mojawapo likiwa la Mitindo la Red Ribbon lililokuwa maalum kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto waliothirika na ugonjwa wa Ukimwi chini ya Taasisi ya Tanzania Mitindo House (TMH) iliyochini ya mwenyekiti, Khadija Mwanamboka.
Katika maonyesho hayo, Jokate pia alikuwa mmoja wa wabunifu wa mavazi ya asili ya Kitanzania yaliyotumia malighafi za Khanga na Vitenge.
“Tunaweza kutumia malighafu za hapa hapa nyumbani kuvaa nguo nzuri, kinachotakiwa ni ubinifu tu, nina kipaji hicho na tayari wadau wameanza kunipongeza kwa kazi nzuri niliyofanya,” anasema na kuongeza:
“Nimeona mwanga katika maonesho ya mitindo japo fani hii bado haijawa na muamko mkubwa, lakini nimeweza kufanya mambo makubwa kama haya.”
Jokate anawashauri vijana kujishughulisha ili kupambana na hali ngumu ya maisha na kuachana na mambo ambayo yanawapotezea muda.
chanzo


KWANINI TUSIMUITE STRONG WOMAN KWA HIKI ALICHO NACHO




Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Search
Popular Posts
-
Akiwa na umri wa miaka 89 aliishi katika kipindi kigumu katika miaka ya 1990 kutokana na talaka za watoto wake 3 na ukimya usiokifani...
-
ALLY REHMTULAH KUJA NA UFAHARI WETU FESTIVAL Mbunifu wa mavazi nchini Tanzania Allyrehmtullah ameandaa tamasha linalokwenda kwa jina ...
-
Msanii wa filamu nchini ambaye pia ni Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu, kufungua duka kubwa la urembo nchini Afrika Kusini. Kwa mujibu wa c...
-
Rangi ya mdomo ni moja ya vipodozi vinavyoongeza urembo kwa mwanamke.Kuna rangi mbalimbali za mdomo kulingana na anachopenda kupaka mrembo h...
-
MISS KINONDONI 2019 PRESS BONANZA Leo miss kinondoni wamefanya special bonanza kwa lengo la kuchangia kituo ch...
-
Tamasha la kutuza watu weusi wanaon"ara kwenye fani tofauti zinazoandaliwa na televison(BET),zilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita na...
-
Huyu ni binti mwenye umri wa miaka19 mzaliwa wa mkoa wa Morogoro amemaliza elimu yake ya msingi na sekondani mkoani morogoro. Fani ya urem...
-
barbra william Hatari sana! Mkali wa Ngoma ya Chekecha Cheketua, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ amenusurika kifo baada ya kuvamiwa nyu...
Recent Posts
Categories
Sample Text
Blog Archive
-
▼
2015
(56)
-
▼
Juni
(10)
- VAZI LA KITENGE
- JOKATE MWENGELO NI MREMBO MWENYE MAFANIKIO MAKUBWA...
- Wema sepetu na mume wa Zari kufungua duka kubwa l...
- Magonjwa ya kinywa na meno husababisha harufu mbay...
- TUMIA MIMEA ASILI KWA KUONDOA CHUNUSI
- Huyu ni mke wa mheshimiwa mmoja hiviiiiiiiii, la h...
- KUWA NA MUONEKANO WA KIPEKEE KATIKA EVENT MBALI MBALI
- UREMBO WA KUCHA KWA MWANAMKE
- Vaa nguo sare na mpenzi wako
- Breaking News; Msanii Maarufu wa Bongo Movie Afari...
-
▼
Juni
(10)
0 maoni:
Chapisha Maoni