Alhamisi, 2 Julai 2015
Asilimia kubwa ya watu wamekuwa na tatizo la kuwa na makovu yanayosababishwa na chunusi kwa kipindi kirefu bila kupata ufumbuzi, na hii husababishwa sana na mabadiliko ya miili kipindi cha ujana , au kwa watu wenye nyuso zenye mafuta na baadhi ya watu wamepata matatizo haya baada ya kutumia baadhi ya vipodozi visivyoendana na ngozi zao. Tatizo hili limekuwa kubwa kwa baadhi ya watu na kuna wakati mtu ana kosa hata raha na kuwa huru kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na mtu kwa kuogopa muonekano wa madoadoa ya ngozi ya uso wake. Leo tutaenda kuangalia moja ya tiba ya kuondoa madoa madoa ya chunusi inayoweza kutengenezwa na mtu yoyote nyumbani bila kutumia gharama kubwa.
Mahitaji
Unga wa Riwa
Maji ya Rose (Rose water)
Maji safi ya kawaida
Limao
Mafuta ya Olive (Olive oil)
Hatua ya Kwanza
Chukua unga wa Riwa na Maji Rose uyachanganye pamoja na ukoroge hadi mchanganyiko wako uwe mzito.
Hatua ya Pili
Upake mchanganyiko wako katika sehemu yenye makovu na uache hadi ukauke. Unaweza kukaa na huu mchanganyiko huu kwa muda mrefu ila inategemea na nafasi yako pia, mchanganyiko huu unasaidia kunyonya mafuta na kuacha ngozi kavu.
Hatua ya Tatu
Nawa vizuri na maji ya uvuguvugu.
Hatua ya Nne
Paka Juice ya Limao kwenye sehemu yenye makovu. Juisi ya limao inatumika kama brichi ya asili ambayo husaidia kufifisha madoadoa na kuondoa makovu kwenye ngozi .
Hatua ya Tano
Paka mafuta ya Olive kwenye makovu, hii husaidia kulainisha ngozi na kufanya makovu yasionekane kirahisi.
Mambo ya kuzingatia
Wakati unaanza kufanya tiba hii jaribu kuacha kutumia aina ya vipodozi vya kemikali ulivyokuwa unatumia na utumiea hii tiba ya asili isiyo na madhara. Jaribu kufanya zoezi hili walau mara mbili kwa wiki ndani ya mwezi mmoja utaona matunda yake.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Search
Popular Posts
-
Akiwa na umri wa miaka 89 aliishi katika kipindi kigumu katika miaka ya 1990 kutokana na talaka za watoto wake 3 na ukimya usiokifani...
-
ALLY REHMTULAH KUJA NA UFAHARI WETU FESTIVAL Mbunifu wa mavazi nchini Tanzania Allyrehmtullah ameandaa tamasha linalokwenda kwa jina ...
-
Msanii wa filamu nchini ambaye pia ni Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu, kufungua duka kubwa la urembo nchini Afrika Kusini. Kwa mujibu wa c...
-
Rangi ya mdomo ni moja ya vipodozi vinavyoongeza urembo kwa mwanamke.Kuna rangi mbalimbali za mdomo kulingana na anachopenda kupaka mrembo h...
-
MISS KINONDONI 2019 PRESS BONANZA Leo miss kinondoni wamefanya special bonanza kwa lengo la kuchangia kituo ch...
-
Tamasha la kutuza watu weusi wanaon"ara kwenye fani tofauti zinazoandaliwa na televison(BET),zilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita na...
-
Huyu ni binti mwenye umri wa miaka19 mzaliwa wa mkoa wa Morogoro amemaliza elimu yake ya msingi na sekondani mkoani morogoro. Fani ya urem...
-
barbra william Hatari sana! Mkali wa Ngoma ya Chekecha Cheketua, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ amenusurika kifo baada ya kuvamiwa nyu...
Recent Posts
Categories
Sample Text
Blog Archive
-
▼
2015
(56)
-
▼
Julai
(11)
- MAYUNGA NALIMI AIRTEL TRACE MUSIC STAR
- JINSI YA KUJIWEKA WA THAMANI KWA MPENZI WAKO
- Miti shamba inayofanya matiti kuwa makubwa na yal...
- JE? UNAMFAHAMU LINAH SANGA NJE NA MUZIC ANAJISHUGH...
- BREAK NEWS;UJIO WA LOWASA CHADEMA WAWAGAWA MBOWE N...
- STAA NA MTOKO TOFAUTI NDANI YA BET
- MNYAMA MWENYE SAUTI KUBWA DUNIANI
- FAIDA YA LIMAO KWENYE NGOZI
- FANGASI SEHEMU ZA SIRI
- PENDEZA KWA KUPAKA MAKE UP KUTOKANA NA KIREMBA ULI...
- CHAGUA RANGI YA MDOMO KUTOKANA NA RANGI YAKO
-
▼
Julai
(11)
0 maoni:
Chapisha Maoni