Jumapili, 26 Aprili 2015

On 07:20 by barbrawilliam in    No comments


square_with_sponsors
Mtangazaji wa redio anayependwa TZW1         
Dida – Times FM
D’Jaro Arungu – TBC FM
Diva – Clouds FM
Mariam Kitosi – Times FM
Millard Ayo – Clouds FM

Kipindi cha redio kinachopendwa TZW2
Ala     za Roho – Clouds FM
Amplifaya – Clouds FM
Hatua Tatu – Times FM
Papaso – TBC FM
XXL – Clouds FM
Mtangazaji wa runinga anayependwa TZW3     
Abdallah ‘Dullah’ Ambua – EATV  
Salama Jabir – EATV/Maisha Magic
Salim Kikeke – BBC Swahili
Sam  Misago – EATV
Zamaradi Mketema – Clouds TV
Kipindi cha runinga kinachopendwa TZW4
Friday Night Live – EATV
In My Shoes – EATV
Mkasi – EATV
Planet Bongo – EATV
Take  One – Clouds TV

Blog/Website inayopendwa TZW5
Muongozaji wa video anayependwa TZW6
Abby Kazi
Adam Juma
Khalfan
Hanscana
Nisher
Muongozaji wa filamu anayependwa TZW7
Jacob ‘JB’  Stephen
Leah Mwendamsoke
Timothy  Conrad
Vincent ‘Ray’  Kigosi
William Mtitu
Muigizaji wa kike wa filamu anayependwa TZW8
Elizabeth ‘Lulu’  Michael
Irene  Uwoya
Jacqueline  Wolper
Riyama  Ally
Wema Sepetu
Muigizaji wa kiume wa filamu anayependwa TZW9
Hemedi  Suleiman
Jacob   ‘JB’    Stephen Mzee
King Majuto
Salim ‘Gabo’ Ahmed
Vincent  ‘Ray’ Kigosi
Mwanamuziki wa kike anayependwa TZW10
Lady  Jaydee
Linah
Mwasiti
Shilole
Vanessa  Mdee
Mwanamuziki wa kiume anayependwa TZW11 
Alikiba
Barnaba
Diamond  Platnumz
Jux
Ommy Dimpoz
Filamu inayopendwa TZW12
Chausiku
Kigodoro
Madam
Mshale wa Kifo
Sunshine
Video ya muziki inayopendwa TZW13
Akadumba –  Nay  wa        Mitego
Kipi Sijasikia – Profesa Jay
Nani kama Mama – Christian Bella f/ Ommy Dimpoz   
Wahalade –  Barnaba
XO – Joh  Makini
TZW Nominees - 2105

Jumatatu, 13 Aprili 2015

On 04:25 by barbrawilliam in    No comments

IMETOSHA yaendeleza mkakati wake kimataifa kusafisha jina la nchi

Mkakati wa kutokomeza unyanyapaa na mauaji ya watu wenye ualbino nchini, uitwao IMETOSHA, juzi ulianza rasmi kujitokeza kimataifa baada ya kushiriki katika pambano la kimataifa la kirafiki kati ya nyota wa zamani wa Barcelona na Veterani wa Afrika Mashariki.
Katika mpambano huo wa kimataifa uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mkangara, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadick na maafisa kutoka katika mkakati huo walipata nafasi ya kuongea na wachezaji hao nyota wa Barcelona kuhusiana na dhana iliyoko katika nchi za nje ambako inaaminika Tanzania wanauana wenyewe kwa wenyewe kutokana na imani za kishirikina.
Akiongea baada ya mpambano huo ambapo Barcelona waliibuka washindi, Balozi na muasisi wa mkakati huo unaoelekea na sura ya kizalendo na kitaifa, Bw. Henry Mdimu alisema kulikuwa na haja wachezaji hawa warudi na ujumbe kwao wenye majibu ya maswali wanayojiuliza kuhusiana na mauaji ya albino na kukosa majibu.
“Maneno haya ya kwamba sisi tunauana kwa imani za kishirikina, ingawa matukio mengi yapo kanda ya Ziwa lakini nchi nzima inachafuka kwa hiyo haja ya kusafisha jina la nchi kwa mataifa ya nje ipo na sisi IMETOSHA tumeamua kuchukua jukumu”, alisema Balozi huyo ambaye pia ana ualbino.
Mdimu alibainisha kwamba katika mkakati wa kimataifa wameanza kwa kuanzisha tovuti (imetosha.or.tz) ambayo itakuwa ikionesha matukio mbali mbali yanayopinga mauaji na unyanyapaa ili wanaoamini vingine waone kwamba unyanyapaa na mauaji kwa watu wenye ualbino si kitu ambacho watanzania kama taifa wanakifurahia.
Balozi huyo pia alitoa wito kwa kila mtanzania kuuunga mkono mkakati wa IMETOSHA ili katika miaka 20 ijayo  kizazi kijacho kiwe na jamii yenye watu wenye ualbino wanaoishi kwa amani katika nchi yao.
Wachezaji wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania wakiongozwa na Patrick Kluivert (aliebeba mtoto) wakiingia uwanjani tayari kwa kukipiga na timu ya Tanzania Veterans katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. hadi mwisho wa mchezo, Barcelona ya Hispania ilishinda bao 2-1.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania, Patrick Kluivert akifurahia jambo na Mtoto Sharifa mwenye Ualbino kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Tanzania Veterans uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. 
 
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mkangara (wa pili kulia) akizungumza jambo na Mchezaji wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania, Patrick Kluivert wakati akiwasalimia wachezaji hao kabla ya kuanza kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Tanzania Veterans, uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jana.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadick.
Sehemu ya Wachezaji wa timu ya Tanzania Veterans na Barcelona wakiwa kwenye picha ya pamoja na Watoto wenye Ualbino mbele ya Bango la Mkakati wa kutokomeza unyanyapaa na mauaji ya watu wenye ualbino nchini, uitwao IMETOSHA. 

Jumapili, 12 Aprili 2015

On 08:29 by barbrawilliam in    No comments

MAGWIJI wa Tanzania wafungwa bao 2-1 na Magwiji wa Tanzania 
Bao la kwanza la Barcelona limefungwa na Luis Garcia katika dakika ya 9′ akimalizia mpira wa kona uliochongwa na mkali wao, Mholanzi, Patric Kluivert.
Tanzania walisawazisha dakika ya 44′ kupitia kwa Yusuph Macho.
Barcelona waliandika bao la pili na la ushindi katika dakika ya 86′ kupitia kwa Kluivert aliyefunga kwa mwakwaju wa penalti baada ya beki Mustapha Hoza kumuangusha Kluivert mwenyewe.
Naodha wa magwiji wa Tanznia akiojiwa na Bwiga wa cloustv na clous fm

Mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo

AY na FID Q ni moja ya washabiki wa Barcelona nao walikuwepo uwanjani na walitupia Jezi za klab hiyo

Mchezaji Patrick Kluvert na wenzake wakiingia uwanjani kupasha kabla ya mechi kuanza

Kocha wa Barcelona akibadilishana mawazo

Blogger na Meneja tv51 Lonely L.Nzali alikuwepo kukupasha Habari

wachezaji wa Barcelona wakionesha upendo kwa walemavu wa ngozi kabla ya mechi kuanza

Waziri wa Habari ,utamaduni na michezo Mh;Fenera Mkangara akisalimiana na wachezaji

Nahodha wa tanzania akionesha kuumia baada ya kufungwa goli la kwanza

Mchezaji wa Barcelona akiteta jambo na chipukizi wa soka Tanzania

Alhamisi, 26 Machi 2015

On 10:39 by barbrawilliam in ,    No comments
Classic Rabia: nguo ndefu ina umuhimu wake kwa mtoko wa usiku: NGUO fupi imekuwa maarufu kwa mitoko ya usiku kwa shughuli mbalimbali, na wadada wengi wamekua wakipendeza sana, lakini hata hivyo wengi wam...

Ijumaa, 13 Machi 2015

On 02:39 by barbrawilliam in    No comments


DSC_0034
Mwanamziki wa Bongo Fleva Linah Sanga leo asubuhi amekula shavu la kuwa balozi wa kinywaji cha JEBEL FULL KIPUPWE. Akiwa katika ofisi za Serengeti Breweries Limited msanii huyo alidondosha wino wa mkataba huo huku akiwa pembeni na Managing Director wa SBL Ndugu Steve Gannon.
Pia Linah amekula mkataba wa mwaka mmoja na kampuni fulani hivi ambayo atakuja kuitamka yeye mwenyewe chini ya mameneja wapya na kampuni hiyo itamghamia kuanzia muziki wake pamoja na video yake mpya anayoenda kuifanya South Africa. Kampuni hiyo imesema inatarajia kutoa shilling Million 270 kwa mwaka huo mmoja watakaokuwa na Linah.
DSC_0067DSC_0075
Pichani kuanzia kushoto ni Managing Director wa SBL Steve Gannon pamoja na meneja wa Linah aliyekaa upande wa kulia wakishuhudia kwa makini wakati Linah akisaini mkataba huo wa kinywaji cha JEBEL FULL KIPUPWE

Jumanne, 3 Machi 2015

On 22:10 by barbrawilliam in    No comments

Tanzania ni moja ya nchi zilizoko chini ya jangwa la sahara afrika imekuwa na wimbi la kuongezeka kwa 
watu wenye ulemavu ngozi ,jamii ya kitanzania imekuwa na imani potofu juu ya watu hawa wengine wakiamini
ulemavu wa ngozi ni kama mkosi.
Miaka ya tisini jamii nyingi zilidanganya  ya kwamba albino aishi na iwa wanapotea lakini kweli nikwamba 
jamii hizo zimekuwa zikiwahua pindi pale tu wanapozaliwa na kuwaficha kwa kuwazika katika mashamba na 
hata ndani ya nyumba zao.
Tanzania imeweza kufumbua macho baada ya uhuru wa vyombo vya habari kuanza kuriport habari za mauji
ya watu hawa nakutoa elimu ya kuwatambua albino kama binadamu wengine na wanaweza fanya kila kitu 
kama binadamu wengine.
Lakini miaka ya 2006 yakaanza kutokea mauaji ya watu hawa tena ikishirikishwa na imani za kishirikina 
kwa baadhi ya watu wakiamini wanapotumia viungo vya albino watafanikiwa katika mambo yao ya Biashara
na hata uongozi hasa katika masuala ya siasa.

Mwenyekiti wa Chama cha albino(W)Temeke Bw; Kassim Kibwe(kushoto) na Mjumbe wa Chama hicho
Bw;Yahya Nakanoga
ndipo harakati za wanahabari kuanza kuliwekea mkazo suala la unyanyasaji wa jamii hiyo ya walemavu wa ngozi
pongezi za dhati ziende kwake Vick mtetema mwanaharakati aliyepigana kufa nakupona kuhakikisha mauaji haya
ya albino yanakwisha nakutokomezwa kabisa ndipo kufanikisha kuanzishwa kwa shirika la "Under the same sun"
ambalo lilikuja kwa nia ya kutetea haki za walemavu hawa na kuwakwamua kiuchumi na hata kielimu.
Lakini licha ya jitiada hizo na walemavu kuwa namategemo juu ya shirika hilo hali imekuwa ndivyo sivyo
baada ya sasa kuonekana shirika hilo likiwa na watu wachache wanaonufaika na misaada hiyo na namba kubwa 
ya watu hao ikibaki ikiwalalamikia viongozi wa shirika hilo Tanzania.

Akiongea nasi Mwenyekiti wa chama cha albino wilaya ya Temeke Bw.Kassim Kibwe anasema shirika la under
the same sun limekuwa likitenda ndivyo sivyo kwa sasa kama awali lilivyokuja nakutokuwa na imani nalo tena
hasa kwa kitendo cha kusambaza fomu kwa wazazi wasiojiweza ili kuwaandikisha watoto wao waweze someshwa 
lakini ajabu ni kwamba unakuta mzazi hana hata pesa ya kununua kiatu cha mtoto na anaambiwa ampeleke mtoto shule ambazo
ni International na under the same sun wanachangia gharama kiasi na huku gharama zinging zikitakiwa kutoka mzazi tena hugo ambaye 
hana uwezo wa kulimia hata mavazi tu ya mtoto kwa shule za kawaida.
Bw;Kibwe (Mkt wilaya ya Temeke) akionesha katiba ya chama cha albino kwa waandishi wa habari
mengi utaendelea kuyapata kupitia online Tv51(www.tv51.co.tz)makala na vipindi kama fahamu kuhusu albino
ikiwa pamoja na matatizo yanayowakabili walemavu wa ngozi Tanzania

Na Lonely L.nzali
Dar es salaam