Alhamisi, 26 Machi 2015

On 10:39 by barbrawilliam in ,    No comments
Classic Rabia: nguo ndefu ina umuhimu wake kwa mtoko wa usiku: NGUO fupi imekuwa maarufu kwa mitoko ya usiku kwa shughuli mbalimbali, na wadada wengi wamekua wakipendeza sana, lakini hata hivyo wengi wam...

Ijumaa, 13 Machi 2015

On 02:39 by barbrawilliam in    No comments


DSC_0034
Mwanamziki wa Bongo Fleva Linah Sanga leo asubuhi amekula shavu la kuwa balozi wa kinywaji cha JEBEL FULL KIPUPWE. Akiwa katika ofisi za Serengeti Breweries Limited msanii huyo alidondosha wino wa mkataba huo huku akiwa pembeni na Managing Director wa SBL Ndugu Steve Gannon.
Pia Linah amekula mkataba wa mwaka mmoja na kampuni fulani hivi ambayo atakuja kuitamka yeye mwenyewe chini ya mameneja wapya na kampuni hiyo itamghamia kuanzia muziki wake pamoja na video yake mpya anayoenda kuifanya South Africa. Kampuni hiyo imesema inatarajia kutoa shilling Million 270 kwa mwaka huo mmoja watakaokuwa na Linah.
DSC_0067DSC_0075
Pichani kuanzia kushoto ni Managing Director wa SBL Steve Gannon pamoja na meneja wa Linah aliyekaa upande wa kulia wakishuhudia kwa makini wakati Linah akisaini mkataba huo wa kinywaji cha JEBEL FULL KIPUPWE

Jumanne, 3 Machi 2015

On 22:10 by barbrawilliam in    No comments

Tanzania ni moja ya nchi zilizoko chini ya jangwa la sahara afrika imekuwa na wimbi la kuongezeka kwa 
watu wenye ulemavu ngozi ,jamii ya kitanzania imekuwa na imani potofu juu ya watu hawa wengine wakiamini
ulemavu wa ngozi ni kama mkosi.
Miaka ya tisini jamii nyingi zilidanganya  ya kwamba albino aishi na iwa wanapotea lakini kweli nikwamba 
jamii hizo zimekuwa zikiwahua pindi pale tu wanapozaliwa na kuwaficha kwa kuwazika katika mashamba na 
hata ndani ya nyumba zao.
Tanzania imeweza kufumbua macho baada ya uhuru wa vyombo vya habari kuanza kuriport habari za mauji
ya watu hawa nakutoa elimu ya kuwatambua albino kama binadamu wengine na wanaweza fanya kila kitu 
kama binadamu wengine.
Lakini miaka ya 2006 yakaanza kutokea mauaji ya watu hawa tena ikishirikishwa na imani za kishirikina 
kwa baadhi ya watu wakiamini wanapotumia viungo vya albino watafanikiwa katika mambo yao ya Biashara
na hata uongozi hasa katika masuala ya siasa.

Mwenyekiti wa Chama cha albino(W)Temeke Bw; Kassim Kibwe(kushoto) na Mjumbe wa Chama hicho
Bw;Yahya Nakanoga
ndipo harakati za wanahabari kuanza kuliwekea mkazo suala la unyanyasaji wa jamii hiyo ya walemavu wa ngozi
pongezi za dhati ziende kwake Vick mtetema mwanaharakati aliyepigana kufa nakupona kuhakikisha mauaji haya
ya albino yanakwisha nakutokomezwa kabisa ndipo kufanikisha kuanzishwa kwa shirika la "Under the same sun"
ambalo lilikuja kwa nia ya kutetea haki za walemavu hawa na kuwakwamua kiuchumi na hata kielimu.
Lakini licha ya jitiada hizo na walemavu kuwa namategemo juu ya shirika hilo hali imekuwa ndivyo sivyo
baada ya sasa kuonekana shirika hilo likiwa na watu wachache wanaonufaika na misaada hiyo na namba kubwa 
ya watu hao ikibaki ikiwalalamikia viongozi wa shirika hilo Tanzania.

Akiongea nasi Mwenyekiti wa chama cha albino wilaya ya Temeke Bw.Kassim Kibwe anasema shirika la under
the same sun limekuwa likitenda ndivyo sivyo kwa sasa kama awali lilivyokuja nakutokuwa na imani nalo tena
hasa kwa kitendo cha kusambaza fomu kwa wazazi wasiojiweza ili kuwaandikisha watoto wao waweze someshwa 
lakini ajabu ni kwamba unakuta mzazi hana hata pesa ya kununua kiatu cha mtoto na anaambiwa ampeleke mtoto shule ambazo
ni International na under the same sun wanachangia gharama kiasi na huku gharama zinging zikitakiwa kutoka mzazi tena hugo ambaye 
hana uwezo wa kulimia hata mavazi tu ya mtoto kwa shule za kawaida.
Bw;Kibwe (Mkt wilaya ya Temeke) akionesha katiba ya chama cha albino kwa waandishi wa habari
mengi utaendelea kuyapata kupitia online Tv51(www.tv51.co.tz)makala na vipindi kama fahamu kuhusu albino
ikiwa pamoja na matatizo yanayowakabili walemavu wa ngozi Tanzania

Na Lonely L.nzali
Dar es salaam