Alhamisi, 10 Septemba 2015

On 13:33 by barbrawilliam in ,    No comments
lulu73268
Msanii wa Movie hapa nchini Elizabeth Michel a.k.a Lulu amefunguka haya mambo matano kuhusu chama anachokipenda na ni nani atampigia kura yake, hii ni baada ya kuona wasanii wengi wakionyesha mapenzi yao katika vyama wanavyo vipenda na wengine kutoa ngoma zinzo sifu vyama vyao.
Na hiki ndicho alicho andika kupitia ukurasa wa Instagram “Okay….nimeulizwa na Wengi na pengine yanasemwa mengi kuhusu ni Chama kipi cha Siasa nina support Kama ilivyoonekana Kwa Wasanii Wenzangu wengine..! Kwa kifupi nitajaribu kufafanua machache Kwa huu uwezo mdogo wa kufikiri nilijaaliwa na Mwenyezi Mungu..!
Kwanza,kila binadamu/mwananchi ana uhuru wa kuchagua na ku support anachokipenda…kwahyo sitangaa wala kuchukia Flani ku support upande flani
Pili,Mimi Kama mm(binafsi)hii ni Mara yangu ya kwanza kupiga kura kwahiyo nimeamua kuitumia Kwa busara na kuifanya iwe na Mafanikio na isiyo na majuto Kwa kutofuata mkumbo wowote wa ndugu,jamaa,marafiki au watu walionizunguka..!
Tatu,Nimependa kuitumia NAFASI hii zaidi Kwa UHUSIKA wa ELIZABETH na sio LULU nikimaanisha ikiwa kila kura ya mwananchi wa wakawaida ni ya siri na kuuridhisha moyo wake basi na mm nitakuwa mwananchi wa kawaida kbsa katika hili..!
Nne,natoa pongezi Kwa wasanii wenzangu waloweza kushiriki Kwa namna moja au nyingine ktk ku support upande mmoja au mwingine kwani wameonyesha ujasiri na mapenzi ya kweli Kwa vyama wanavyo support ILA tu mabishano ya HOJA ni mazuri zaidi na yanaweza kuepusha ugomvi au kuvunja mahusiano yetu ambayo yalikuwepo kabla ya UCHAGUZI na yatatakiwa kuendelea kuwepo baada ya UCHAGUZI..!
Tano,Nawatakia Kila La kheri Wagombea wote na Natumaini Uchaguzi utakuwa wa SAWA na HAKI..! Mwisho,mimi nimejiandikisha na nina KIKATIO changu
tayari,napenda kuwahimiza wananchi/WaTanzania wenzangu kujitokeza katika uchaguzi ili kumchagua yule unayeona anakufaa….tuombe Mungu na Tujitahidi uchaguzi uwe wa Amani na tuepuke maneno au vitu Vyovyote vinavyoweza kuashiria kuleta vurugu katika uchaguzi wetu Mkuu…!
MunguIbarikiTanzania
KuelekeaUchaguziMkuuOctober2015
KuraYanguSiriYangu
Elizabeth Michael ‘Lulu’ “elizabethmichaelofficial” on Instagram

0 maoni:

Chapisha Maoni