Ijumaa, 13 Machi 2015

On 02:39 by barbrawilliam in    No comments


DSC_0034
Mwanamziki wa Bongo Fleva Linah Sanga leo asubuhi amekula shavu la kuwa balozi wa kinywaji cha JEBEL FULL KIPUPWE. Akiwa katika ofisi za Serengeti Breweries Limited msanii huyo alidondosha wino wa mkataba huo huku akiwa pembeni na Managing Director wa SBL Ndugu Steve Gannon.
Pia Linah amekula mkataba wa mwaka mmoja na kampuni fulani hivi ambayo atakuja kuitamka yeye mwenyewe chini ya mameneja wapya na kampuni hiyo itamghamia kuanzia muziki wake pamoja na video yake mpya anayoenda kuifanya South Africa. Kampuni hiyo imesema inatarajia kutoa shilling Million 270 kwa mwaka huo mmoja watakaokuwa na Linah.
DSC_0067DSC_0075
Pichani kuanzia kushoto ni Managing Director wa SBL Steve Gannon pamoja na meneja wa Linah aliyekaa upande wa kulia wakishuhudia kwa makini wakati Linah akisaini mkataba huo wa kinywaji cha JEBEL FULL KIPUPWE

0 maoni:

Chapisha Maoni