Jumatatu, 13 Julai 2015

On 08:38 by barbrawilliam in ,    No comments
Hali ndani ya chadema imezidi kuwa tete mpaka sasa baada ya katibu mkuu wa Chadema Dr.slaa kutishia kurudisha kadi ya Chadema  na kuachana na siasa za chama hicho kama MBOWE ataendelea kumshawishi na kumuomba LOWASA kujiunga na chama hicho ili awe mgombea wao wa uraisi.
Dr.SLAA ameonyesha msimamo huo muda mfupi kabla ya LOWASA hajaongea na waandishi wa habari nyumbani kwake masaki kuhusiana na hatima yake hiyo.Slaa amekihakikishia chambo  chetu kwamaba yeye hamuungi mkono MBOWE kwenye mpango wake huo wa kumtaka LOWASA awe mgombea wa urahisi kupitia chama hicho.
Kijana mmoja wa CHADEMA ambaye yupo karibu na MBOWE amethibitisha kwamba MWENYEKITI wao huyo yupo tayari hata kumfukuza chama SLAA ili LOWASA  awe mgombea wao anasema MBOWE anaamini kwamba LOWASA ataipeleka CHADEMA madarakani
Kwasababu ya mpasuko huo,timu ya mkakati ya LOWASA imeamua kuahirisha  mkutano wao na Waandishi wa Habari uliokuwa ufanyike leo saa tano asubuhi hii kama ambavyo Mbowe ameomba ili kwanza wamalize tofauti zilizojitokeza kati yake na SLAA.Ikumbukwe kwamba  hivi sasas SLAA ana mvutanao mkubwa na viongozi wenzake wa UKAWA ambapo analazimisha yeye awe mgombea.

Tayari  mzee EDWIN MTEI ametumiwa  ndege ili aje Dar haraka kumshawishi SLAA akubali kumpisha LOWASA kugombea urais

Jumatatu, 6 Julai 2015

On 06:01 by barbrawilliam in ,    No comments
Tamasha la kutuza watu weusi wanaon"ara kwenye fani tofauti zinazoandaliwa na televison(BET),zilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita na kukusanya  idadi kubwa ya watu maarufu kutoka barani America na Africa.

Tukio hili muhimu duniani lilifanyika katika ukumbi wa MicrosoftTheatre,Los Angeles na kutoa fursa kwa mastaa kupata tuzo ikiwa ni ishara ya kutambuliwa  kwa mchango mkubwa katika sekta tofauti Kama kawaida ya shughuli hizo,watu maarufu walitumia kwa malengo tofauti,hasa kwa kuonyesha mitindo mbali mbali ya nguo,nywele,viatu nk
 baadhi ya mastaa waliopita kwenye zulia jekundu la shughuli hiyo muhimu ni pamoja na mastaa wengi kupendeza katika stly ya kipekee
  nick minaj alivaa gauni jeusi lililofuata mwili wake wakati naturi naughton alivaa la mackenzie lililobuniwa na kyemar mcentyre, ambaye alistua mitandao alipobuni  vazi lake mwenyewe lililo mithili ya tarumbeta.
On 03:24 by barbrawilliam in ,    No comments
Je? unamfahamu nyama mwenye sauti kubwa duniani kuliko wengine,leo nakujuza kupitia safu hii ya TUJUZANE.Nyangumi ndiye mnyama mwenye sauti kubwa kuliko kituchochote  duniani.Hutoa sauti kali sana kipimo cha decibles188 ambayo inaweza kusikika  mpaka umbali wa kilomita 848.
Ni sauti kubwa kuliko sauti yaitoayo ndege kubwa aina ya JET inapopaa angani ambayo kipimo cha sauti ya JET ni decubles 120.

Alhamisi, 2 Julai 2015

On 04:23 by barbrawilliam in , ,    No comments
How to Get Rid of Pimple Scars Naturally
Asilimia kubwa ya watu wamekuwa na tatizo la kuwa na makovu yanayosababishwa na chunusi kwa kipindi kirefu bila kupata ufumbuzi,  na hii husababishwa  sana na mabadiliko ya miili kipindi cha ujana , au kwa watu wenye nyuso zenye mafuta na baadhi ya watu wamepata matatizo haya  baada ya kutumia baadhi ya vipodozi visivyoendana na ngozi zao. Tatizo hili limekuwa kubwa kwa baadhi ya watu na kuna wakati mtu ana kosa hata raha na kuwa huru  kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na mtu kwa kuogopa muonekano wa madoadoa ya ngozi ya uso wake. Leo  tutaenda kuangalia  moja ya tiba ya kuondoa madoa madoa ya chunusi inayoweza kutengenezwa na mtu yoyote nyumbani bila kutumia gharama kubwa.

Mahitaji
Unga wa Riwa
Maji ya Rose (Rose water)
Maji safi ya kawaida
Limao
Mafuta ya Olive (Olive oil)

Hatua ya Kwanza
Chukua unga wa Riwa na Maji Rose uyachanganye  pamoja na ukoroge hadi mchanganyiko wako uwe mzito.

Hatua ya Pili
Upake mchanganyiko wako katika sehemu yenye makovu na uache hadi ukauke. Unaweza kukaa na huu mchanganyiko huu kwa muda mrefu  ila inategemea na nafasi yako pia, mchanganyiko huu unasaidia kunyonya mafuta na kuacha ngozi kavu.

Hatua ya Tatu    
Nawa  vizuri na maji ya uvuguvugu.

Hatua ya Nne
Paka Juice ya Limao kwenye sehemu yenye makovu.  Juisi ya limao inatumika kama brichi ya asili ambayo husaidia kufifisha madoadoa  na kuondoa makovu kwenye ngozi .

Hatua ya Tano
Paka mafuta ya Olive  kwenye makovu, hii husaidia kulainisha ngozi na kufanya makovu yasionekane kirahisi.


Mambo ya kuzingatia
Wakati unaanza kufanya tiba hii jaribu kuacha kutumia aina ya vipodozi vya kemikali ulivyokuwa unatumia na utumiea hii tiba ya asili isiyo na madhara. Jaribu kufanya zoezi hili walau mara mbili kwa wiki  ndani ya mwezi mmoja utaona matunda yake.
On 01:58 by barbrawilliam in    No comments
Maambukizi ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa na uwepo wa fangasi wanaojulikana kitaalamu kama Candida albicans. Maambukizi haya pia hujulikana kama yeast infection au thrush. Fangasi hupatikana kama vimelea vya kawaida katika mdomo, mpira wa kupitisha chakula sehemu inayojulikana kama pharynx, katika kibofu cha mkojo, uume na hata kwenye uke.
Mfumo mzuri wa kinga wa mwili pamoja na  aina fulani za bakteria wanaoishi pamoja na fangasi husaidia sana katika kuthibiti maambukizi yanayoyosababishwa na aina hi ya fangasi.
Kwa kawaida, Candida albicans huishi kwenye uke na sehemu nyingine kama zilivyoelezewa hapo juu bila kusababisha madhara yoyote yale isipokuwa pale mazingira ya  eneo husika yanapobadilika kama vile mabadiliko katika hali ya PH ya eneo husika (ifahamike ya kwamba pH ya kawaida ndani ya uke ni 4.0 – 4.5) au uwiano wake na vimelea (microorganisms) lakini pia uharibiwa kutokana na sababu mbalimbali kama vile matumizi ya madawa aina ya antibiotics na kupungua kwa kinga mwilini kutokana na magonjwa mbalimbali n.k.
Maambukizi haya ya fangasi yanaweza kugawanywa katika sehemu kuu mbili;
  1. Maambukizi yasiyo makali yaani ‘uncomplicated thrush’ kwa kiingereza:
  2. Maambukizi makali yaani ‘complicated thrush’ kwa kiingereza:
Kwa kawaida Watu walio katika hatari ya kupata maambukizi ya fangasi hawa ni wale wenye;
  • Kutumia sana dawa aina ya detergents kwenye sehemu za siri au douches (vifaa vinavyotumiwa kusafishia uke kwa kutumia maji yaliyochanganywa na jiki au antiseptic yoyote ile) kwa sababu hali hiyo husababisha kuharibika kwa uwiano wa fangasi na aina nyingine ya vinyemelezi kama bakteria aina ya lactobacilli
  • Kutumia sana madawa aina ya antibiotics, steroids ambayo yana tabia ya kushusha kinga ya mwili
  • Ugonjwa wa ukimwi (HIV/AIDS) n.k
ANGALIZO Wanawake wenye umri wa miaka kati ya ishirini na thelathini wapo kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi haya wakati wale ambao wameshaacha kupata hedhi au wale ambao hawajaanza kupata hedhi kabisa hawako kwenye hatari kubwa.
Dalili na viashiria kwa wanawake;
  • Kuwashwa sehemu za siri (kwenye tupu ya mwanamke)
  • Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri (burning sensation)
  • Kufanya kama vidonda katika sehemu za siri (soreness)
  • Maumivu wakati wa kujamiana (superficial dyspareunia)
  • Maumivu au usumbufu wakati wa kujisaidia haja ndogo (wakati mtu anakojoa)
  • Kuvimba na kuwa rangi nyekundu kwa mdomo wa nje wa tupu ya mwanamke (labia minora)
  • Kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au nyeupe kijivu, unaoweza kuwa mwepesi, majimaji au mzito na ambao umefanana na jibini (cottage cheese like discharge) wenye muonekano unaojulikana pia kama curd-like appearance. Kwa kawaida, uchafu huu haumbatani na harufu yoyote isipokuwa panapokuwa na tatizo la ziada kama ugonjwa wa zinaa aina ya Bacteria vaginosis. Uchafu huu unaotoka hapa unaweza kuenea kwenye maeneo mengine yaliyokaribu na tupu ya mwanamke kama kwenye mitoki (groin area) au perineum na kusababisha kuharibika kwa ngozi katika sehemu hizo.
Dalili na viashiria hivi huwa mbaya zaidi wakati mwanamke anapokaribia kupata hedhi.
Dalili na viashiria kwa wanaume ni;
  • Kuwashwa sehemu za siri
  • Kuvimba na kuwa rangi nyekundu kwenye ncha ya uume
  • Kuwepo kwa uchafu wa rangi nyeupe (kama nilivyoeleza hapo juu) kwenye sehemu ya juu ya uume.
  • Kuwa na vidonda vidogo kwenye uume (sore on the glans)
Hata hivyo, mara nyingi wanaume hawaoneshi dalili zozote zile, ni vizuri kwa mwanamke kumueleza mwenza wake pale anapopata maambukizi haya ili naye pia apate kutibiwa.

Jumatano, 1 Julai 2015

On 11:52 by barbrawilliam in    No comments

On 11:27 by barbrawilliam in , ,    No comments
Rangi ya mdomo ni moja ya vipodozi vinavyoongeza urembo kwa mwanamke.Kuna rangi mbalimbali za mdomo kulingana na anachopenda kupaka mrembo husika.Kwa mujibu wa wataalamu wa masuara ya urembo unaweza kupaka rangi ya mdomo kulingana na umri,tukio na nguo unazovaa au ulizo vaa siku hiyo
Katika safu hii ya urembo leo nitakujjuza namna ya kuchagua rangi ya mdomo kulingana na umri wako.

           *Wasichana wanashauriwa kupaka rangi za kawaida











*wanawake wanafanya kazi wanashauriwa kutokupaka rangi zinazo ng"ara au zilizokolea wakati wanakwenda kazini.*

    *Wanawake vijana wenye ngozi angavu na umri18na25wanashauriwa kupaka rangi ya pinki.
    *Wanawake wenye ngozi nyeusi kati  ya 18na25wanaweza kupaka rangi za machungwa
     *Wanawake wenye umri25na40 wanashauriwa kupaka rangi zilizopoa.                          .
















Kwa kufanya hivyo,siku zote utajikuta ukiwa na mvuto kwa rangi ya mdomo hata kama una umri mkubwa