Jumanne, 16 Septemba 2025
On 00:27 by barbrawilliam No comments
Faida za kutumia ua la Ulimi wa Mama Mkwe kiroho ni nyingi sana, hasa kwa mtu mwenye macho ya rohoni au anayejishughulisha na mambo ya kinga ya kiroho, usafi wa hewa ya kiroho (energy), na ulinzi wa nyumba au biashara. Huu mmea ni maarufu sana kwa uwezo wake wa kuvuta nguvu chanya na kufukuza hasi.
🌟 FAIDA ZA KIROHO ZA ULIMI WA MAMA MKWE:
1. Kinga dhidi ya nguvu za giza
Ua hili linaaminika kuwa ngao dhidi ya uchawi, husuda, mikosi, majini, mizimu mibaya, na roho za kishetani.
Linafyonza mitetemo mibaya na kuzuia viumbe wa kiroho wabaya kuingia nyumbani au kazini.
2. Kuvunja laana na mikosi
Kwa wenye bahati mbaya ya mara kwa mara (kazi kufa, fedha kupotea, afya kuyumba pasipo sababu ya kimwili), ua hili huweza kusaidia kubadili hali hiyo.
Watu wa rohoni hutumia mmea huu kuvunja vifungo vya kiroho (spiritual bondages) kwa kuweka majani yake kwenye maji ya kuoga au kwenye pembe za nyumba.
3. Kulinda mlango dhidi ya nguvu hasi
Ukiliweka kwenye mlango wa kuingilia nyumba au biashara, huzuia mtu mwenye roho chafu au mawazo ya kuharibu kuingia.
Hii ni kwa sababu lina nguvu ya kutambua na kukataa mitetemo mibaya.
4. Kuvuta bahati njema (positive energy)
Ulimi wa Mama Mkwe huleta bahati, ustawi, na mafanikio unapowekwa sehemu za kazi au biashara.
Husaidia kufungua njia zilizofungwa kiroho, hasa kwa watu wanaojitahidi lakini mambo hayaendi.
5. Kuimarisha nguvu ya maombi au ibada
Unapoweka mmea huu karibu na sehemu ya maombi, unaweza kusaidia kusafisha hewa ya kiroho na kuondoa usumbufu wa kipepo au mivuto mibaya.
Unaweza kuomba ukiwa karibu na mmea huu ili kusafisha mazingira ya kiroho.
🛡️ JINSI YA KUTUMIA KIROHO:
Weka kwenye kona 4 za nyumba kwa ajili ya ulinzi wa pande zote.
Weka mlangoni upande wa ndani au nje ili kuzuia roho chafu.
Oga kwa majani yake yaliyochemshwa (ikiwezekana kwa ruhusa ya kiroho), ili kuvunja vifungo na kuondoa mikosi.
Ongea maneno ya baraka au dua unapoliweka, ukilielekeza kufanya kazi ya kiroho unayotaka (mfano: “nakutuma ulinde nyumba yangu dhidi ya husuda na laana…”).
Kumbuka: Mambo ya kiroho hutegemea sana imani, nia, na usafi wa moyo. Kama una macho ya rohoni, utaweza kuhisi au kuona mwenyewe jinsi linavyofanya kazi.
Jumatatu, 10 Aprili 2023
Jumanne, 21 Machi 2023
On 07:10 by barbrawilliam No comments
washiriki wa mkutano wa kujadili masuala ya matumizi ya Nishati safi na salama kwenye Magari mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo Machi 21, 2023.
WADU wa Usafiri kutoka nchi 17 za Kikanda Afrika wajadili masuala ya matumizi ya Nishati safi na salama kwenye Magari hapa nchini jijini Dar es Salaam leo Machi 21, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akimwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Angela Kairuki akizungumza wakati wa kufungua kikao kazi hicho amesema kikao kazi hicho kitajadili masuala ya matumizi ya umeme kwenye magari pamoja na matumizi ya betri ili kuepukana na uchafunzi wa mazingira na hali ya hewa.
Amesema magari yanayotumia umeme yatasaidia katika utunzaji wa mazingira na kuzuia uharibifu wa hali ya hewa ili kuendana na sera ya dunia inavyopambana na kukabiliana na uchafuzi wa mazingira.
Kwa upande wa Afya amesema kuwa Usafiri huo utaoanzia jijini Dar es Salaam utapunguza jamii kupata matatizo ya afya yanayotokana na uchafunzi wa hali ya hewa pamoja na kupunguza gharama za matibabu ya maradhi mbalimbali hasa yanayosababishwa na uchafuzi wa hali ya hewa.
Kwa Upande wa teknolojia ameeleza kuwa jamii inatakiwa kuwa na uelewa thabiti katika matumizi ya magari ya umeme ambapo kutatakiwa kuwe na muendelezo wa miundombinu pamoja na kuachana teknolojia ya kutumia mafuta ya magari.
"Hii ni mhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania pamoja na kupunguza gharama kwa utumiaji magari ya Umeme."
Magari ya usafiri wa umma yanawajibika na unachangia asilimia 67.4 ya uchagunzi mazingira unaotokana na hewa ukaa.
Akizungumzia kuhusiana na mradi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Makalla amesema kuwa kunafaida kubwa za kujenga miundombinu jijini Dar es Salaam kwa sababu inasaidia wananchi kupata usafiri wa uhakika na kubeba watu wengi kwa wakati mmoja.
Amesema kuwa sekta ya usafiri inachangia kuleta uharibifu wa mazingira unaotokana na hewa ya Kabonidayoksaidi.
Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Dkt. Edwin Mhede amesema kuwa katika Mjadala watajadili namna nchi za Afrika zinaweza kuja na matumizi ya magari yanayotumia nishati rafiki ili kupunguza kiwango cha hewa ya ukaa ambayo huzalishwa kila uchwao kutoka kwenye magari yanayotumia nishati ya mafuta.
Amesema mkutano huo unalenga kujadili kubadili matumizi ya mabasi au magari yanayotumia nishati ya umeme katika majiji yanayoendelea katika nchi za kikanda za Afrika.
Amesema nishati ya umeme inatoa kiwango cha kabonidayoksaidi kwa kiwango cha sifuri kwasababu kunakuwa hakuna makelele wala uchafunzi wa hali ya hewa.
Akizungumzia kuhusiana na Changamoto zilizopo amesema kuwa uelewa wa jamii ni mdogo na Kila jambo linaeleweka kwa kujifunza na kupeana elimu, pia amesema kuanachangamoto za kimuundo ambapo changamoto hizo zinahitaji sera za uhakika, kama sera za kisheria, za kikodi na sera za uwekezaji, sera za fedha.
"Mazingira hayo lazima yafungamanishwe yote ili kutoa motisha ya wawekezaji ambao wanaweza kuwekeza kwenye sekta ya uzalishaji wa magari au watakao agiza magari kutoka nje ya nchi kule nchini kwaajili ya kutoa huduma.
Hata kwa Sisi waendeshaji tunahitaji kupata mazingira wezeshi ya kisera, ambayo yatapelekea kuona thamani ya fedha iliyowekezwa." Amesema Dkt. Mhede
Akizungumzia mradi wa BRT Dkt. Mhede amesema kuwa mtaji mkubwa uliopo Dar es Salaam ni miundombinu kukua kwa kasi na 'icon' Nembo ya BRT Afrika amesema ipo Dar es Salaam pia kwasiku moja wanahudumia watu zaidi ya laki mb
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akizungumza wakati wa kufunguzi kikao kazi cha washiriki kutoka nchi 17 wakijadili masuala mbalimbali ya matumizi nishati safi katika magari. Kikao kazi hicho kimefunguliwa leo Machi 21, 2023 jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Dkt. Edwin Mhede, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kufunguliwa kwa kikao kazi cha wawakilishi kutoka nchi 17 za kanda ya Afrika wa kujadili masuala ya matumizi ya Nishati safi na salama kwenye MagaPicha ya pamojaMwakilishi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Rwanda, Janvier Twagirimana akizungumza wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya matumizi ya Nishati safi na salama kwenye Magari. Pia ameelezea namna usafiri nchini Rwanda unavyofanya kazi ikiwa ni pamoja kutumia Baiskeli zinazotumia umeme
On 06:54 by barbrawilliam No comments
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Komred Abdulrahman Kinana afungua Mafunzo ya Umoja wa wanawake wa Tanzania (UWT) kwa Wajumbe wa Baraza kuu ,Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa na Wilaya katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.
*WAELEZENI MAZURI YALIYOFANYWA NA RAIS Dk. SAMIA KUTEKELEZA ILANI YA CCM: KINANA*
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amewataka viongozi wa CCM wayaeleze kwa wananchi mambo mazuri yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Kinana aliyasema hayo jijini hapa jana, wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kuanzia ngazi ya Taifa hadi Wilaya.
“Katika maeneo yenu hakikisheni mnakisemea Chama na mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia, wala msione haya kusema ili wananchi wajue na hata katika chaguzi zijazo tusipate shida.
Alisisitiza kuwa: "Chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia katika kipindi cha miaka miwili kila kata kuna alama ya maendeleo kuanzia shule, zahanati, barabara na maendeleo ya watu, tuna kila sababu ya kujisifia na kuusifia uongozi wa mwenyekiti wa chama hiki."
Vilevile, Kinana aliwataka viongozi wa UWT kubeba ajenda za wanawake kitaifa bila kuogopa jambo lolote.
KUHUSU UCHAGUZI
Akizungumzia kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, Kinana aliwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ili kufia lengo la kujenga jamii yenye usawa.
Alisema mwakani kuna uchaguzi wa viongozi wa serikai za mitaa, hivyo ni vyema wanawake wakajitokeza kuchukua fomu kuomba nafasi mbalimbali za uongozi na CCM itawapa ushirikiano wa kutosha.
“Kuelekea uchaguzi ujao jiandaeni na kuwahimiza wanawake kuwania nafasi zote za uongozi na ninawahakikishia kuwa, CCM itawaunga mkono kwa hali na mali ili kuwa na wanawake wengi waliochaguliwa katika majimbo,”alisema.
ASISITIZA VIKAO
Katika hatua nyingine, Kinana aliwataka UWT kuhakikisha maamuzi mengi yanafanyika kupitia vikao na sio maamuzi ya mtu mmoja au kikundi cha watu.
Alisisitiza kuwa hata kiongozi anapokosea sio busara kumuamisha kituo cha kazi kabla ya kumuita na kumsikiliza kwani utakuwa ni ukiukwaji wa haki.
“Niwasihi tumieni vikao kuamua mambo sio kikundi cha watu, kila kitu lazima kijadiliwe kwa kina na kipite kwa hoja kwa sababu ndani ya CCM hakuna maamuzi ya mtu mmoja au amri, ninyi katika maeneo yenu hakikisheni ndani ya vikao huko ndio haki ya mtu itapatikana.
“Wenyeviti mpunguze kuhamisha watu hovyo, kama mtu amekosea aitwe aelezwe kosa sio kuchukua maamuzi ya haraka una muhalibia mtu mwelekeo, tujenge utamaduni wa kuambiana ukweli na msiogopane mtu anapokosea,”alisema.
Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM aliwashauri viongozi kusoma vitabu mbaimbali vya Chama ikiweo Ilani ya uchaguzi, sera, kanuni na katiba kwani vitawasaidia katika masuala mbalimbali ya uongozi.
Alisema CCM ni miongoni mwa vyama vichache duniani ambayo vinamaandishi mengi.
“Someni katiba, kanuni, ilani na sera kwani vitawasaidia kuendesha shughuli mbalimbali za Chama na kuongoza kwa kuzingatia misingi ya haki,”alisema
UWT WAELEZA
Awali, Mwenyekiti wa UWT Taifa, Marry Chatanda, alisema wanawake wanaridhika na kazi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia kwani ilani ya CCM inatekelezwa kwa kishindo.
Alisema katika kipindi cha miaka miwili ya serikali ya awamu ya sita hakuna kilichosimama ndio maana waliandaa hafla ya kumpongeza Rais Dk.Samia kwa kazi nzuri alizozifanya.
“Sisi wanawake wa CCM hakika tumeridhishwa na uongozi wa Rais Dk.Samia na tunaahidi katika uchaguzi wa mwaka 2025 tutatoa fedha kwa ajili ya kumchukulia fomu mwanamke mwenzetu,”alisema.
Kwa upande wake, Katibu wa UWT Taifa Dk. Philis Nyimbi alisema lengo la mafunzo hayo ni kuleta ustawi na kuwapatia viongozi maarifa namna ya kuongoza jumuiya hiyo katika ngazi zote.
Alisema mafunzo hayo yamewakutanisha viongozi 478 ambapo baada ya kumaliza elimu waliyoipata wataipeleka katika ngazi ya kata na matawi.
“Mafunzo haya ni mahususi kwa ajili ya kuwajengea uwezo viongozi wetu ukizingatia tunaelekea katika uchaguzi mkuu mwaka 2025, hivyo kutokana na mafunzo haya watatakiwa kuyapeleka katika ngazi ya kata na matawi na kutuletea taarifa,”alifafanua.
On 06:29 by barbrawilliam in Habari No comments
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema kuwa Bandari Kavu ya Kwala
inatarajiwa kuanza kufanya kazi muda wowote kuanzia sasa na itatoa huduma zote za
kiforodha kama zinavyotolewa katika Bandari zingine.
Akizungumza hivi karibuni kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa,
Meneja Miliki wa Mamlaka hiyo, Alexander Ndibalema ameeleza kuwa, kukamilika kwa
bandari hiyo ni matokeo chanya ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita ambayo
imewezesha takriban Shilingi bilioni 83.247 kutumika katika kuendeleza bandari, ujenzi wa
barabara ya zege yenye urefu wa kilometa 15.5 kutoka barabara kuu ya Morogoro eneo la
Vigwaza kuelekea bandarini na kusogeza miundombinu ya reli mchepuko yenye urefu wa
kilometa 1.3.
"Bandari Kavu ya Kwala ipo tayari kufanya kazi kwa sababu miundombinu yote ya msingi
imekamilika na leseni zingine kutoka mamlaka zingine za Serikali zimeshakamilika ambapo
kinachosubiriwa kwa sasa ni kupata leseni kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)",
alisema Ndibalema.
Ndibalema ameongeza kuwa, lengo kuu la kuanzisha bandari hiyo ni kuongeza ufanisi na
kiasi cha shehena inayohudumiwa katika bandari ya Dar es Salaam, kupunguza msongamano
katika bandari ya Dar es Salaam, kuongeza mapato ya Serikali kupitia huduma zitolewazo
katika Bandari. Hivyo wateja kutoka sehemu mbalimbali wataweza kuchukulia mizigo yao
ndani ya bandari hiyo ambayo ina uwezo wa kuhudumia wastani wa makasha 823 kwa siku
sawa na makasha 300,395 kwa mwaka sawa na asilimia 30 ya makasha yote
yanayohudumiwa katika Bandari ya Dar es Salaam kwa sasa.
Vile vile amefafanua kuwa, bandari hiyo ni ya kimkakati kwa sababu eneo la Kwala lina
miradi mingi ya kimkakati ambayo imeanza kutekelezwa ikiwemo ujenzi wa viwanda
mbalimbali na ujenzi wa Mji mpya wa Kwala, hivyo ni matarajio kuwa mizigo ya Wawekezaji
kutoka nchi mbalimbali inayokwenda kwenye viwanda itachukuliwa hapo.
Ameeleza kuwa, bandari hiyo inatarajiwa kuchangia kwa kiwango kikubwa katika Pato la
Taifa ambapo sehemu kubwa ya mizigo itakayohudumiwa katika bandari hiyo ni ile
inayokwenda nchi jirani.
Bandari hiyo imejengwa kwa awamu mbili zilizojumuisha usafishaji wa eneo lenye ukubwa
wa Hekta 60 na ujenzi wa ukuta uliogharimu Shilingi 9,465,643,798.00, ujenzi wa Yadi hekta
5 kiwango cha zege uliogharimu Shilingi 36,670,971,842.00, ujenzi wa Reli Mchepuko yenye
urefu wa KM 1.3 uliogharimu Shilingi 677,328,320.00 na ujenzi wa barabara yenye urefu wa
KM 15.5 kwa kiwango cha zege uliogharimu Shilingi 36,432,867,115.70 ambayo imekamilika
kwa asilimia 100.
Alhamisi, 2 Februari 2023
On 08:27 by barbrawilliam No comments
Katika kuadhimisha miaka 46 ya chama Cha mapinduzi wanachama wa UWT Turiani wilaya ya mvomero wameshiriki upandaji wa miti karibu na mto mbulumi uliopo tarafa ya Turiani wilaya ya Mvomero ili kusaidia kuzuia madhara yanayotokana na kufurika kwa mto huo kipindi Cha mvua
Sambamba na hilo mwenyekiti wa UWT ambaye pia ni mgeni rasmi wa maadhimisho hayo ndugu Rachel Steven Kingu ameongoza ugawaji wa vifaa mbalimbali vya usafi katika zahanati ya Turiani wilaya ya Mvomero ikiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha vituo vya afya nchini.
Aidha ndugu Kingu ameshiriki zoezi la ugawaji wa kadi za Chama Cha Mapinduzi kwa wanachama wapya na kutoa hamasa kwa viongozi wa ngazi zote hasa madiwani kushirikiana na serikali katika kufanikisha adhma ya chama na serikali kwa ujumla
On 04:43 by barbrawilliam No comments
On 04:38 by barbrawilliam No comments
On 04:23 by barbrawilliam No comments
Jumatano, 1 Februari 2023
On 22:29 by barbrawilliam No comments
On 21:14 by barbrawilliam No comments
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kufanya uchunguzi wa bili na bei za maji kwa wananchi wilayani Malinyi mkoani Morogoro ili kupata ukweli iwapo wananchi hao wanabambikiwa bili au lah.
Kauli hiyo ameitoa leo katika Kata ya Mtimbila aliposimamishwa na wananchi akiwa katika msafara wake kuelekea Makao Makuu ya Wilaya ya Malinyi kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kama ilivyoahidiwa kwenye Ilani ya CCM.
Mara baada ya kusimamishwa eneo hilo na wananchi walitoa kero yao kuwa bili ya maji ni sambamba na gharama za kununua maji ambapo pamoja na kwamba chanzo cha maji ni cha mserereko lakini bado wanatozwa shilingi 100 kwa ndoo ya lita 20.
Aidha,wamema bei ya maji wanayotozwa kwa mwezi kwa wale ambao hawajafungiwa mita za maji za ni shilingi 7,000 na bili hiyo inalipwa kila mwezi hata kama maji hayatoki.
Akijibu kero hiyo ambayo pia imetolewa na wananchi katika Wilaya ya Kilombero,Chongolo aliagiza Takukuru kufanya uchunguzi ili kuona uhalali wa bei hizo kwani mwongozo wa malipo ya maji ya chanzo hicho ni shilingi 20, kwa ndoo moja ya maji ya lita 20.
“Takukuru,hili lichukueni lichunguzeni kuona uhalali wake,maana nimepewa kero hii mara nyingi,sasa lifanyieni kazi,”amesema Chongolo.
Chongolo yupo katika ziara ya kikazi mkoani Morogoro akiwa ameongozana na Katibu wa Halmashauri Kuuya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema na Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Haji(Gavu)
Jumanne, 28 Desemba 2021
Jumatatu, 27 Desemba 2021
On 22:21 by barbrawilliam in Habari No comments
Mwanamuziki maarufu Defao Desemba 03, 2018, alikuwa ni mwenye furaha ya kutimiza miaka 60 tangu azaliwe.
Licha ya umri huo kuwa mkubwa, ukimuona jukwaani ama kwenye Luninga hauwezi kuamini kama ana uwezo wa kulichezesha tambo lake lililojaa minofu kila sehemu.
Defao alizaliwa Desemba 03, 1958 katika jiji la Kinshasa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Baada ya kuzaliwa akapewa majina ya Mutomona Defao Lulendo.
Ni mwanamuziki mwenye talanta za kutunga na kuimba kwa sauti nyembeba na nyororo.Defao aliaza kujishughulisha na muziki mwaka 1976, akiwa katika bendi ya Orchestra Suka Movema. Baadae akaenda kujiunga katika bendi ya Fogo Stars.
Mwaka 1978 Defao akaenda kupiga muziki katika bendi ya Korotoro huko Somo, Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).Alikuwa mmoja kati ya wanamuziki waliounda bendi mpya ya Grand Zaiko Wawa mwaka 1981, ikiongozwa na mpiga gitaa mashuhuri Pepe Felix Manuaku.
Katika kile kilichoitwa mbinu za kujitafutia maisha, Defao aliungana na mwanamuziki Ben Nyamabo kuunda kikosi kipya cha Choc Stars.Bendi hiyo ya Choc Stars na Orchestra Shakara Gagna Gagna, zilikuwa chini ya uongozi wa Jeanpy Wable Gypson, zilimfanya General Defao kuwa maarufu kwa mara kwanza kitaifa.
Akiwa na wanamuziki akina Ben Nyamabo, Debaba, Carlito, Bozi Boziana na Djuna Djunana, bendi ya Choc Stars ikajizolea umaarufu mkubwa kupitia tungo zao.Uimbaji na uwajibikaji jukwaani wa General Defao aliweza kuonesha kuwa kipaji chake siyo cha kubahatisha.
Defao Mutomona kwa kawaida hucheza sambamba na wanenguaji wake, ambapo huwa kivutio kikubwa cha wapenzi na mashabiki wake akicheza mitindo mbalimbali ukiwemo ule wa ‘Ndombolo’ pasipo kuchok
Mutomona ilipofika mwishoni mwa mwaka 1990, aliiacha bendi hiyo ya Choc Stars, akiwa na madhumuni ya kuunda bendi yake.Dhamira yake alitimia baada ya kuunda bendi yake iliyopewa jina la Big Stars.
Katika bendi hiyo hupiga muziki kwa kushirikiana na mwimbaji mwingine Djo Poster, aliyetokea katika bendi ya Grand Zaiko.Defao aliomuongeza katika safu ya wanamuziki mpiga solo chipukizi Jagger Bokoko, ambaye alitokea kuwa kipenzi chake kikubwa.
Bendi ya Big Stars ilikuwa na wanamuziki wengi wenye uwezo mkubwa wa kutengeneza muziki.Kulikuwa na waimbaji akina Djo Djo Bayenge, Debleu Kinanga na Adoli Bamweniko.Kwa upande wa wapiga magitaa, kulikuwa na Mogus aliyekuwa akilicharaza gitaa la solo, gita la besi likiungurumishwa na Guy wa Nzambi.
Tumba zilikuwa zikidundwa na Richa Cogna Cogna. Mbofya kinanda alikuwa ni Sedjo Kavanda.Katika kipindi cha miaka mitano ya bendi ya Big Stars, Defao alionesha ubunifu uliomletea mafanikio makubwa baada ya kufyatua album zisizopungua 17. Kati ya hizo, sita ziliingia katika soko la Ulaya mwaka 1995.
Mifarakano katika sehemu za kazi huwa hazikosi. Big Stars iliteteleka kwa kipindi kifupi mara baada ya kuondoka Djo Djo Bayenge na kumuacha Defao akiwa kiongozi wa bendi hiyo.Defao akiwa na wanamuziki wake wa Big Stars, walikarabati upya bendi yao na kuweza kutengeneza kikosi kipya chenye wanamuziki mahiri. Walimuongeza Roxy Tshimpaka.
Roxy kabla ya kujiunga na Big Stras alikuwa katika bendi ya Choc Stars. Aidha alimpata mwimbaji mpya Azanga.Siku zilivyokuwa zikiiendela, mpigaji gitaa la solo Jagger Bokoko akawa kuwa kipenzi kikubwa cha Defao.
Umaarufu wa General Defao ulizagaa maeneo mengi Afrika Mashariki na Kati kwenye miaka 1990.
Wapenzi na mashabiki wake waliulingaisha umaarufu wake na ule wa wanamuziki akina Papa Wemba, Koffi Olomide, Bozi Boziana na Kester Emeneya.Hapana ubishi kwamba Defao Mutomona ni mwanamuziki aliye na umaarufu mkubwa miongoni mwa wanamuziki toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mpenzi msomaji utakubaliana nami iwapo utasikiliza nyimbo za Georgina, Fammilie Kikuta, Nadine, Bana Kongo, Oniva na Filie.Nyimbo hizo ziko katika kiwango cha juu na zimepigwa katika mitindo miwili ya rumba na sebene mold.Kufuatia uangalizi wa uzalishaji wa kazi toka kwa meneja wake kuwa mbovu, Defao hulazimika kubadili maprodyuza na kampuni za kurekodia.
Wakati mwingine alikuwa akitoka na matoleo ya kazi zake zilezile kwa lebo tofauti.Defao alilivunja kundi zima la Big Stars mwaka 2000 wakiwa katika jiji la Kinshasa.Yeye akaamua kwenda ‘kutanua’ katika jiji la Paris nchini Ufaransa wakati wa kipindi cha joto.Lakini akiwa katika jiji hilo, alirekodi album ya Nessy de London, akiwashirikisha wanamuziki nyota waishio katika jiji hilo la Paris.
Wanamuziki hao walikuwa akina Nyboma Mwandido, Luciana de Mingongo, Wuta Mayi, Ballou Canta na Deesse Mukangi, walioshirikiana na Defao kufanya onesho kubwa lililo wavutia watu wengi.Defao kwa kuwatumia waimbaji hao waalikwa, walipelekea album yake ya De London kupanda chati zaidi.
Aliachia album nyingine nyingi zikiwa na nyimbo za Mandova, Ya Gege, Copinnage, Sam Samita, Salanoki Guerre De1, Animation na Nessy of London.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Defao baadae akawa kimya katika anga ya muziki.Hali hiyo yasemekana kuwa ilitokana na sintofahamu ya kisiasa nchini mwake iliyopelekea kufungiwa kupiga muziki huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa uongozi wa Rais Lauler Kabila.
Defao alifika nchi za Afrika ya Mashariki ikiwemo Tanzania.Katika ziara yake ya humu nchini iligubikwa na matatizo lukuki mwaka 2000, uliokuwa mwaka mpya wa Millenium.Baada ya kumaliza kufanya maonyesho kadhaa, Defao alizidiwa akili na ‘Mapromota’ waliomleta, matokeo yake alifikia hadi kukosa pesa ya kujikimu pamoja na kulipia Visa yake kuwa mushkeri.
Nguli huyo ‘alifulia’ hata nauli ya kumrejesha kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hakuwa nayo.Bahati njema ilikuwa upande wake kwa kuwa alifanikiwa kurejea kwao baada ya kupewa ‘lift’ katika ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATC), aliyokuwa ikizindua safari zake kati ya Dar es Salaam na Lubumbashi nchini DRC.
“Kimya kingi kina mshindo mkuu” usemi huu ulijionesha wazi kwa gwiji hilo lililosubiriwa na wapenzi kwa kipindi kirefu hadi mwaka 2006, ndipo alipotoka na album yake mpya yenye Lebo ya Nzombo le Soi.
Baada ya miaka minne mingine alifyatua CD yake yenye Lebo ya Pur Encore mwaka 2010.Mwaka 2012 Defao kwa bahati nzuri alirudi uliongoni akiwa na album ya The Undertaker.Defao pamoja na kuadhimisha miaka yake 60, amekuwa kimya hadi leo bila ya kutoka na album nyingine mpya licha ya kushughulika na muziki akiwa katika nchini kwao DRC na Ulaya.
Mwanamuziki huyo mwaka jana 2018, alikuwa akisikika akifanya maonyesho katika jiji la Nirobi nchini Kenya.
Jumatano, 14 Julai 2021
Hii ni baada ya taarifa siku ta jana kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na watu wengi kushangaa kwanini Miss Tanzania 2020-2021 Rosey Manfere hajatangazwa kwenda kushiriki Miss World2021 na badala yake ametangazwa mshindi wa pili ambaye ni Juliana Lugumisa taarifa za ndani zina sema
"Kulitokea na utovu wa nidhamu kati ya Miss Tanzania Rosey na waandaaji wa mashindano ya miss Tanzania hivyo kutokana na kukiuka baadhi ya taratibu kamati ya Miss Tanzania ikafikia hatua hiyoya kumtangaza mshindi wa pili kwenda kushiriki
Miss Tanzania Rosey Manfere alipewa taarifa wiki mbili zilizopitz kuwa hatoenda kushiriki miss world kutokana na utovu wa nidham"
Taarifa za ndani zinasema hivyo,
Ikumbukwe Miss World 2021 inategemea kufanyika December 16,2021 Puerto Rico na anayepeperusha bendera yetu kwa sasa ni Juliana Lugumisa aliyekuwa Miss Tanzania namba mbili. Waswahili wanasema kutesa kwa zamu
Alhamisi, 18 Julai 2019
Tarehe kama ya leo julai 18 mwaka 1918 alizaliwa,Mzee Nelson Mandela Raisi wa kwanza wa Africa kusini alichaguliwa kidemokrasia na ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel
alifariki December 5-2013 akiwa na umri wa miaka 95.Mandela alitumikia kifungo cha miaka 27 gerezani kwa sababu ya mapambano yake dhidi ya mfumo wa kibaguzi wa adrica kusini unaofahamika kama Ukaburu
Aliachiwa huru kutoka gerezani mwaka 1990 na kuwa raisi alitumikia miaka mine na baadae kuachia madaraka baada ya kutumikika kwa kipindi kimoja tu.Kitendo adimu kufanywa na viongozi waliopo
.
Akiwa mtu anayependwa Zaidi duniani,mandela aliwavutia mamilioni ya watu kwenye hotuba zake zilizokuwa zimejaa maneno ya faraja na ukombzi

Hii ni moja ya nukuu zake alipoamua kuachia madaraka kwa hiyari yake
"ongoza kutokea nyuma na wafanye wengine waamini wao ndio wako mbele zako"
Je?wew unwkumbuka nukuu gani kutoka kwa hayati "NELSON MANDELA"
toa comment yako hapo chini.HAPPY BIRTHDAY NELSON MANDELA
alifariki December 5-2013 akiwa na umri wa miaka 95.Mandela alitumikia kifungo cha miaka 27 gerezani kwa sababu ya mapambano yake dhidi ya mfumo wa kibaguzi wa adrica kusini unaofahamika kama Ukaburu
Aliachiwa huru kutoka gerezani mwaka 1990 na kuwa raisi alitumikia miaka mine na baadae kuachia madaraka baada ya kutumikika kwa kipindi kimoja tu.Kitendo adimu kufanywa na viongozi waliopo
.
Akiwa mtu anayependwa Zaidi duniani,mandela aliwavutia mamilioni ya watu kwenye hotuba zake zilizokuwa zimejaa maneno ya faraja na ukombzi

Hii ni moja ya nukuu zake alipoamua kuachia madaraka kwa hiyari yake
"ongoza kutokea nyuma na wafanye wengine waamini wao ndio wako mbele zako"
Je?wew unwkumbuka nukuu gani kutoka kwa hayati "NELSON MANDELA"
toa comment yako hapo chini.HAPPY BIRTHDAY NELSON MANDELA

Jumatano, 17 Julai 2019
FAHAMU NJIA ZA ASILI ZA KUTIBU VIPELE VYA CHUNUSI KWENYE USO
Habbat sawadah ya unga iliyo sagwa.nusu kikombe ya maganda ya komanga yaliyo sagwa,nusus kikombe ya siki ya tofaha{apple}
MATAYARISHO NA MATUMIZI
Changanya na pasha moto kwa dakika mbili kikombe kimoja cha habbat-dawdaa iliyosagwa nusu kikombe,kikombe cha maganda ya komamanga yaliyosagwa nusu,kikombe cha siki ambayo inatokana na juisi ya tofaha{apple}.Paka katika sehemu inayotakia kabla ya kwenda kulala kila siku usiku mpaka chunusi zitakapoondoka
NB;Mchanganyiko unaweza kukaa mpaka wiki tatu na ni laziam uwekwe kwenye sehemu ya ubaridi
ALLY REHMTULAH KUJA NA UFAHARI WETU FESTIVAL

Mbunifu wa mavazi nchini Tanzania Allyrehmtullah ameandaa tamasha linalokwenda kwa jina la UFAHARI WETU "urith wetu"lenye lengo la kuitangaza utanzania katika vazi la kitenge
Mbunifu huyo wa mitindo ya kipekee nchini amesema maonyesho hayoyatafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini dar es salaam tarehe20 jumamosi hii kwa kuwashirikisha wabunifu na wanamitindo kutoka nchini china pamoja na watanzania ikiwa ni kutangaza Utanzania katika vazi la kitenge
Amewataka wadau mbalimbali kutoa ushirikiano kwa kuleta bidhaa zao siku iyo na watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha ilo la Ufahali wetu 'urith wetu

wabunifu wa mavazi nchini wamejitokeza kutoa ushirikiano pamoja na waandaaji wa vipindi vya urembo na mitindo nao watoa surpot yao siku ya tamasha hilo
m

Mbunifu wa mavazi nchini Tanzania Allyrehmtullah ameandaa tamasha linalokwenda kwa jina la UFAHARI WETU "urith wetu"lenye lengo la kuitangaza utanzania katika vazi la kitenge
Mbunifu huyo wa mitindo ya kipekee nchini amesema maonyesho hayoyatafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini dar es salaam tarehe20 jumamosi hii kwa kuwashirikisha wabunifu na wanamitindo kutoka nchini china pamoja na watanzania ikiwa ni kutangaza Utanzania katika vazi la kitenge
Amewataka wadau mbalimbali kutoa ushirikiano kwa kuleta bidhaa zao siku iyo na watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha ilo la Ufahali wetu 'urith wetu

wabunifu wa mavazi nchini wamejitokeza kutoa ushirikiano pamoja na waandaaji wa vipindi vya urembo na mitindo nao watoa surpot yao siku ya tamasha hilo
m
Jumamosi, 29 Juni 2019
MISS KINONDONI 2019 PRESS BONANZA Leo miss kinondoni wamefanya special bonanza kwa lengo la kuchangia kituo cha watoto yatima Amana centre kilichopo mwananyamala jijini dar es salaam kwa kuosha magari ambayo yana lipiwa na wadau ambao wameweza kujitokeza siku ya leo na kuoshwa na washiriki wa miss kinondoni wakiongozwa na mratibu wao Nancy supermodel na pesa kukusanywa na mlezi wa kituo hicho
Mratibu wa miss Kinondoni Bi Nancy supermodel

Mratibu wa mashindano ya miss Kinondoni 2019 Bi Nancy Supermodel ametangaza rasmi zawadi ya mshindi wa kwanza hadi wa tano,mshindi wa kwanza atajinyakulia zawadi ya gari aina ya bm mini cooper,mshindi wa pili atapata set bedroom,mshindi watatu anapata tv flatscreen kubwa na kin'gamuzi,mshindi wa nne atapata milioni moja,na watano atapata tsh laki tano
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)
Search
Popular Posts
-
Faida za kutumia ua la Ulimi wa Mama Mkwe kiroho ni nyingi sana, hasa kwa mtu mwenye macho ya rohoni au anayejishughulisha na mambo ya kinga...
-
ALLY REHMTULAH KUJA NA UFAHARI WETU FESTIVAL Mbunifu wa mavazi nchini Tanzania Allyrehmtullah ameandaa tamasha linalokwenda kwa jina ...
-
JACKSON KABIRIGI'S PROFILE
-
UREMBO ni jambo muhimu kwa mwanamke kwa kujiweka nadhifu wakati wote ikiwa ni pamoja na kujipamba na kujifanyia usafi wa mwili. Watu wengi w...
-
Fainali ilikua ni Jumamosi ya April 18 2015 ambapo shindano la Airtel Trace Music Stars lilifanyika Nairobi Kenya likiwa ni shindano ...
-
Msanii Linah Sanga alimaarufu kama Ndege mnana amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye nje ya kazi yake ya sanaa ni msusi mzuri wa nywele na al...
-
urembo Fashionable lineup ... Rihanna, Beyonce, Jay Z, Kim Kardashian, Jennifer Lopez and Sarah Jessica Parker. Pictures: Getty Source...
-
Magadi Soda: Magadi soda ni mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Changanya kiasi kidogo cha magadi so...







































